Gwiji
la Muziki wa kizazi kipya Seleman Msindi 'Afande Sele, baba Tunda'
ameamua kuweka wazi sababu inayomfanya ajitose kwenye kinyanyiro cha
kuwania Ubunge jimbo la Morogoro Mjini, kwakuwa watu ambao aliwaamini
mwanzoni kwamba huenda wakawa chanzo cha kupata nafuu kwenye tasnia hiyo
inayopendwa na vijana wengi lakini imekuwa tofauti sana
Afande alisema miongoni mwa watu aliwaowategemea sana na ambao pia
walikuwa kwenye tasnia hiyo ni wanamuziki Joseph Mbilinyi 'Sugu' na
Captain John Komba, ambao aliamini huenda wangeleta mabadiliko kwakuwa
wametokea kwenye fani hiyo. Alisema lakini tangu waingie huko, wamevaa
uhusika wa kisiasa na kila jambo wamekuwa wakilipeleka kisiasa. Hali
iliyompelekea kujipanga kwenda mwenywe bungeni, kupitia chama chochote
cha upinzani, ambacho kitampa uhuru wa kuongea na kufanya yale ambayo
anayahitaji yeye kwaajili ya watu wake. Pia alisema ananafasi nzuri ya
kuwania akiwa mgombea binafsi, mwaka 2015 ambapo uchaguzi mkubwa
utafanyika wa kuwania wabunge na raisi.
|
No comments:
Post a Comment