Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Sunday, June 10, 2012

Taifa Stars yatupa raha........


Timu ya Taifa ya Tanzania Almaarufu kama TAIFA STARS siku ya leo tar 10 june, 2012. ilileta raha kwa watanzania baada ya kuwatoa kimasomaso kwa kuifunga timu ya Gambi kwa Magoli 2 kwa 1.


katika mpambano huo ambao ulikuwa ni wa vuta nikuvute Gambia walikuwa wa kwanza kuchezea nyavu za watanzania mnamo dakika ya 8 kipindi cha kwanza na kuwafanya watanzania kukosa nguvu kabisa ya kushangilia.


lakini nawasifu sana watoto wa KIM POULSEN kwani walicheza kwa kujituma karibia muda wote na kuwashambulia wagambia hao kwa takribani kipindi chote cha kwanza hadi kwenda mapunziko.

waliporudi kipindi cha pili Mashabiki walionekana kuwahimiza sana wachezaji kwa kuwafokea mara walipoona wanaleta mpira wa kuridhika badala ya kushinda magoli.

Chapombe aliwainua watanzania kwa mpira wa kichwa ambao ulijaa wavuni mnamo kipindi cha pili na kuamsha ari kwa watanzani.

Injini ya Jiji nikifuatilia kwa Umakini zaidi Mpambano

Shukrani zimuendee tena kijana wa kitanzania anekipiga Trout Pousant (TP) MAZEMBEkatika nchi ya kidemokrasia ya Kongo, MBWANA SAMATA baada ya kumlamba chenga Beki wa Kushoto wa Gambia mpaka akakaa chini na kutia majalo iliyomfanya beki aliyekuja kusaidia kuitoa  kwa mkono na kuwa Penati iliyotupatia goli la kuongoza

Dokii nae alikuwepo


Napenda kuwashukuru watanzania wenzangu tuliojitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu yetu ya Taifa na naomba kuwapa ushauri ushindi huu usitufanye tujione kama sisi ndo tunajua soka saaaaana mpaka tukashindwa hata kupiga dandana katika mechi zinazokuja, naomba tukaze buti na kuongeza soka kabambe zaidi ya hili tulilolionesha siku ya leo.

TANZANIA OYEEEEEEEEEE!

wakati wa mapumziko huwa tunapata burudani mbalimbali



napenda sana kuona akina dada wakiwa wanajituma sio wanaume peke yetu ndo tunaweza kufanya mambo kama haya...







No comments:

Post a Comment