Kampuni ya TBL kupitia kinywaji chake cha Grand Malt, wanatarajia kuzindua bonge la Tamasha la wazi litakalojulikana kama Grand Malt Tanzania Open Film Festival, ambalo litafanyika mkoani Tanga katika viwanja vya Tangamano kuanzia saa 10; jioni na kuendelea juni 30 hadi julai 6 mwaka huu . Tamasha hilo litakutanisha wasanii wakali kutoka Bongo Movie, pamoja na wanamuziki wa Baikoko, Taarabu na wanamuziki wengine. Tamasha hilo litafanyika kwa muda wa siku saba mfurulizo, huku likiandaliwa na kampuni ya kutengeneza, na kuandaa matangazo ya radio, terevisheni, muziki filamu, pamoja na Mabango, Sofia Production. tamasha la Grand Malta Tanzania Open Film Festival linatarajia kuwafanya Watanzania, kutambua umuhimu wa kazi zao za filamu na kurudisha uzalendo. Kiingilio ni BULEEEE.. Karibu. |
No comments:
Post a Comment