SIRI imefichukua kuwa madai kwamba ‘kichaa’
wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ ni memba wa jamii ya siri
inayodaiwa kumwabudu shetani, Freemason a.k.a Wajenzi Huru zilianza kitambo
lakini sasa zimeshika kasi baada ya kunaswa kwa picha inayomuonesha
akisalimiana na mtasha kwa ishara ya Kifreemason.
Picha ya tukio hilo lilijiri nchini
Uingereza, mwaka jana Diamond alipokwenda kwa ajili ya kufanya tamasha.
Inasadikiwa kwamba mavazi anayotumia
mwanamuziki huyo kuwa ni meusi, yalifanana sawia na yale ya mtasha,
yanayoelezwa kuwa sehemu ya mavazi yanayotumiwa na jamii ya Freemason.
Ishara nyingine ya salamu ya wawili hao
ambayo ilitengeneza nembo ya Freemason ya bikari kwa namna walivyogusanisha
vidole vyao.
Wadau waliyoiona picha hiyo kupitiamtandao wa
kijamii wa Twitter, wanasema kwamba Diamond amekuwa na ishara nyingine
nyingi za aina hiyo hali inayopelekea kuzua utata na kuamini kwamba ni memba wa
jamii hiyo ya Siri.
|
No comments:
Post a Comment