Chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania Sports Writter
Association 'TASWA', jana kilikuwa kikitoa tuzo kwa wanamichezo
mbalimbali ambao wameweza kuitangaza nchi na kuisaidia kukuwa kwa
michezo hiyo. Wanamichezo mbalimbali walipewa tuzo hizo, wakiwemo wale
wa kutoka Zanzibar, na wa hapa Tanzania bara. Katika tuzo hizo mgeni
rasmi alikuwa rais mstaafu wa awamu ya pili, Ndugu Ali Hassan Mwinyi,
wakati tuzo ya Heshima ikienda kwa Timu ya Taifa ya Tanzania ya Taifa
Stars ambayo ilifanya vizuri mwaka 1979 na kufuzu kuingia katika ligi ya
Afrika 1980 histori ambayo imejijenga hadi leo. |
No comments:
Post a Comment