IKIWA kesho kutwa (Juni 16)
ndio pazia la Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS) linafunguliwa rasmi kwa kuanza
kutafuta vipaji mkoani Dodoma
ambapo maelfu ya watu wameonesha nia ya
kujitokeza kushiriki.
Mkoani hapa vijana wengi wameonesha
kuwa na shauku kubwa ya kusubiria kushiriki katika usaili huo ambapo unaanza
rasmi keshokutwa (Jumamosi ya Juni 16) katika ukumbi wa Royal Village.
Shauku hiyo inaweza kuwa
inasababishwa na dau la zawadi la milioni 50 lililotangazwa na kampuni ya simu
za mkononi ya Zantel lakini pia dili la kuendelezwa kisanii ambalo nalo
linawavutia vijana zaidi.
Akizungumzia usaili wa kesho
kutwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampun ya Benchmark Production Ritha Paulsen
alisema kuwa usaili wa mwaka huu watachukua washiriki kuanzia miaka 16 na
kuendelea.
Alisema kuwa uamuzi huo wa
kuchukua washiriki wa kuanzia miaka 16 ni kuwapa nafasi wale wenye uwezo wa
kuimba na kupanga sauti ili nao wajaribu bahati yao.
“Najua kwa mwaka huu kwa kuwa
shindano hili linadhaminiwa na Zantel hivyo mambo yamekuwa ni makubwa zaidi na
napenda kuwaomba vijana kujitokeza kwa wingi zaidi kutumia fursa hii ambayo
Zantel inawapatia mwaka huu” alisema Ritha.
Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa
Zantel Ali Bin Jarsh akizungumzia shindano hilo alisema kuwa Zantel inatambua nafasi ya
muziki katika kukuza ajira na nchini. Alisema kuwa Zantel imeamua
kupitia Epiq Bongo Star Search kuinua vipaji vya vijana katika muziki ikiwa
pamoja na kuwatengenezea njia ya
mafaniko.
Mwisho
|
No comments:
Post a Comment