SHINDANO
kubwa la kutafuta, kuibua na kuendeleza vipaji nchini kwa sasa linaamia mkoani
Lindi katika ukumbi wa Police Officers Mess Jumamosi ijayo. Katika
ukumbi huo washiriki wanatarajiwa kuanza usaili kuanzia saa moja asubuhi ambapo
kabla ya kuanza kuonesha vipaji vyao mbele ya majaji.
Akizungumzia
usaili wa Lindi Jaji Mkuu wa EBSS Ritha Paulsen alisema kuwa kama ilivyokuwa
mkoa wa Dodoma na kisiwani Zanzibar kwa
mkoa wa Lindi wanatarajia kuona vipaji lukuki na aliwasihi wasichana kujitokeza
kwa wingi. “
Mimi ninaamini kuwa mkoa wa Lindi kuna vipaji yani kama ambavyo tumeona kwa
maeneo mengine sasa kwa Lindi nadhani kutakuwa na ushindani mkali kwa kuwa wapo
baadhi ya wasanii kutoka Lindi ambao wameweza kufanya vema katika medani ya
muziki nchini”alisema Ritha.
Akizungumzia
washindi waliopatikana Dodoma na Zanzibar Ritha alisema kuwa wamekuwa wakiimba
vizuri na walionehsa uwezo mkubwa katika kupangilia sauti zao. Naye
Mkuu wa mawasiliano wa Zantel Awaichi Mawalla alisema kuwa Zantel ikiwa kama
mdhamini mkuu wa EBSS 2012 kutokana na imani yao kwa wakazi wa Lindi katika
kuendeleza sanaa anaamini kuwa mbali na kujitokeza kwa wingi ila pia
watadhihirisha kuwa muziki ni asili yao.
Mpaka
sasa majaji wa shindano hilo la EBSS 2012 wameshapata vipaji kutoka Dodoma na
Zanzibar ambapo vijana 10 wamepatikana.
|
No comments:
Post a Comment