WAKATI filamu za DJ Ben na Taxi Driver zikiendelea
kuwa gumzo, mkongwe Steven Jacob `JB’ anayemiliki kampuni ya utengenezaji
filamu ya Jerusalem anakusudia kuibuka na filamu mpya, Vita Baridi
itakayoshirikisha mastaa wa nchi nne tofauti.
Ameiambia
safu hii kuwa, kwake itakuwa filamu ya kwanza kukutanisha wasanii wakali kutoka
katika nchi tofauti na inayozungumzia mapenzi kwa namna tofauti.
“Ni
filamu ambayo imeigizwa na kuzungumzia mapenzi katika mtindo ambao hakuna mtu angefikiria kama upo namna hiyo,” alisema
JB aliyewataja wasanii walioshirikishwa ni Cassie Kabwita wa Zambia, Patcho
Mwamba wa Demokrasia ya Kongo ambaye
anafanya kazi ya muziki nchini, Makombora wa Zanzibar, JB mwenyewe na Kajala
wanatoka Tanzania Bara.
|
No comments:
Post a Comment