Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Monday, March 5, 2012

Sony Music yathibitisha kuchakachuliwa kwa Nyimbo za Michael Jackson


Sony imesema baadhi ya nyimbo za Michael Jackson zimeibwa baada ya tovuti yao kuchakachuliwa.
Kampuni imesema haitothibitisha ni vitu gani au Nyimbo ngapi ambazo zimechukuliwa baada ya shambulio hilo kupitia njia ya Mtandao.
Mwaka 2010 Sony Music ililipa kiasi cha dola za kimarekani milioni 250 ($250 million) (£158m) amabazo ni sawa na Tsh Bilioni 382 na ushehee hv kwa Hayati MJ kwa dili la kipindi cha miaka 7 ili kuwa na hatimiliki ya nyimbo zilizosalia za Michael Jackson.
Nyimbo ya kwanza kutolewa ilipoachiwa albam ya posthumous iliitwa Michael hiyo ilikuwa ni December mwaka huohuo.
Mwanamuziki huyo ambaye alifariki dunia Juni 2009 akiwa na umri wa miaka 50 alirekodi nyimbo mbalimbali ambazo hazikuachiwa hewani na wanamuziki kama Freddie Mercury na Muimbaji wa kundi la Black Eyed Peas Will.i.am.
April mwaka jana Mtandao wa Sony Playstation ulichakachuliwa na kampuni ilikubali na kusema ya kuwa Taarifa binafsi za watu wapatao milion 70 zilichukuliwa kwa ajili ya uchunguzi wao.
Tovuti ya Sony Music pia inashikilia nyimbo za wanamuziki mbalimbali wakiwemo Foo Fighters, Olly Murs na Avril Lavigne ingawa bado haijafahamika kama nao wameathiriwa kutokana na uharifu huo.
Watu wawili kutoka Uingereza waliofikishwa mahakamani kushitakiwa kutokana na uharifu kwa njia ya Kompyuta wamekana mashitaka yao kwa kutumia Kompyuta vibaya hasa kwa ajili ya uharifu na utumiaji wa nyaraka zenye Hatimiriki mtandaoni pasipo ruhusa.
James Marks, 26 kutoka Daventry, na Kijana wa miaka  25 James McCormick kutoka Blackpool, wote wamekamatwa mwezi wa tano mwaka jana na wanatarajiwa kupandishwa kizimbani kutokana na jaribio lao ifikapo January 2013.

USHAURI:
Sasa ndugu yangu Mtanzania unaependa ku-Download download vijinyimbo mtandaoni baada ya wachakachuaji kuchakachua na kuacha watu wajichukulie tu, usije na wewe ukawa umehusika na taarifa zako watu walizipata je utaweza kulipa Faini ukiambiwa Ulipe Bilion 260 fedha ambazo sawa na walizoiba vigogo wa EPA wapatao 10 hapa bongo teh teh teh, mi simo tumieni Kompyuta jamani kwa uangalifu

HALUAAAAAAAAA!

No comments:

Post a Comment