Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Monday, March 5, 2012

Andre Villas Boas(AVB), Kibarua chaota nyasi






Goli lililofungwa na McAuley wa West Bromwich albion bdakika za lala salama lilikuwa Talaka tosha ya Roman Abramovich kwa aliyekuwa Kocha mkuu wa chelsea Mreno Andre Villas Boas ambaye maendeleo yake na timu yake ya chelsea yalikuwa Mabovu.


Chelsea ilivunja mkataba wa AVB toka porto ambapo alikuwa na mafanikio ya kucheza mechi za msimu mzima wa ligi ya Porto na Klabu ndogo ya Uropa bila hata kufungwa kitu kilichomfanya Abramovich aamini kocha huyo anaweza kuleta neema katika timu yake ya chelsea lakini mambo yamekwenda ndivyo sivyo.

Hivyo basi abramovich ameamua kuvunja tena Mkataba wake na Kocha huyo na hivyo kuamua mikoba ya kocha mkuu wa klabu kushikiliwa na Kocha aliyekuwa Mchezaji wa timu hiyo kipindi cha nyuma na liyekuwa Pia Msaidizi wa AVB muitaliano Roberto Di Matteo.


Lakini Darubini yangu mzee wa Injini  ya jiji CLOUD 112 nimeangaza mpaka kwenye ubongo wa Abramovich ambaye ameonekana kuvutiwa sana na baadhi ya makocha ambao alijaribu kuongea nao ili wakaimu mikoba hiyo ambao ni



JOSEP (PEP) GUARDIOLA

Huyu ni kocha ambaye anaonekana kuwa na uhakika wa kufundisha soka kwani kwa sasa kikosi chake Cha Barcelona kimekuwa tishio sana Hapa duniani kiasi cha kila timu anayokutana nayo zimekuwa zikicheza kwa hofu ya kufungwa kutokana na soka la hawa jamaa.


RAFA BENITEZ


Kocha huyu alikuwepo katika ligi ya Uingereza kipindi cha nyuma ambapo naye alikuwa na wakati mgumu kutokana na Mafanikio madogo na kuyumbayumba na timu aliyokuwa nao kwa wakati huo timu ya Liverpool. Lakini alipoondolewa na kwenda italy (Inter Milan) alifanikiwa kuonesha makali yake lakini  hakuwa na Bahati ya kufanya vizuri kama wenye timu walivyokuwa wanategemea hivyo aliachishwa kazi.


Mimi kama mdau namba MOJA wa Chelsea Hapa Nchini ningemshauri Bosi wangu wa timu Amchukue Pep Guardiola  au aliyekuwa natimu hiyo kabla ya PEP, Frank Rijkaard ambaye nadhani ndiye aliyeleta mafanikio yote ambayo sasa unayaona wanayo Timu ya Barcelona. Haya jamani msinicheke na timu yangu kwani ndo mpira huo Mambo yatakaa Vyema tu

HALUAAAAAAAAAAAA!

No comments:

Post a Comment