NYOTA wa muziki wa dansi ambaye pia ni kiongozi wa bendi ya FM Academia, Nyoshi El Saadat,
amekamilisha kutengeneza video ya wimbo wake unaokwenda kwa jina la OTILIA, huku akisema ameifanya kwa gharama kubwa katika nchi mbalimbali za Ulaya ikiwamo Ubelgiji, Uholanzi na Ufaransa.
Nyoshi alisema kwamba akiwa Uholanzi alifanya kazi na Kampuni ya Makoma, ya Gwiwizambi ambaye alikuwa akifanya kazi na Defao. Alisema alikwenda kufanya mastering na video katika nchi hizo ili kufanya video zake ziwe na kiwango cha kimataifa.
Hata hivyo aliongeza kwa kusema video hiyo itawasili nchini mwishoni mwa mwezi huu.
kwa wale ambao ni wadau wakubwa wa Nyoshi mnaombwa muweke macho katika mkao wa kula.
HALUAAAAAA!
No comments:
Post a Comment