Mwanamuziki wa kizazi kipya wa Bongo Flava LINAH juzi Alhamis ya Tarehe 1 Mwezi huu wa Tatu alikwea Pipa kuelekea Nchini Marekani ambapo atakuwa na ziara ya Miezi miwili katika miji tofauti Nchini humo akinadi sauti yake Kimuziki.
Mwanadada huyu (LINAH) ataanza na shoo yake ya kwanza Houston na itakayofuatia katika jiji la Dalas ambayo itakuwa ni siku ya Pasaka kisha itafanyika shoo nyingine katika jiji la DC ambayo ni kwa ajili ya VIJIMAMBO BLOG ambayo inatimiza miaka 4.
Linah atafanya pia shoo mbalimbali akiwamo katika Nchi hiyo ya marekani kikubwa ni kwamba Injini ya jiji nina Furaha ya kuona nyota ya Tanzania iking'aa katika Nchi za Mbali kupitia Anga ya Muziki. Ninachoweza sema ni kwamba napenda Kumpongeza mwanadada Linah kwa juhudi zake za Kuendeleza Kipaji chake cha Muziki na Kueperusa Bendera ya Nchi yetu na kutoa Changamoto kwa wasanii wengine ambao nao wanatamani kufikia walau Mafanikio hayo.
Mungu akupe Nguvu na Ujasiri wa kufanya zaidi ya kile Ulicho nacho LINAH!
Haluaaaaaaa!
MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment