Meli iitwayo Gold Star imekamatwa karibu na pwani ya Italy ikiwa
na zaidi ya tani 30 za dawa za kulevya ambapo Polisi wa Italy wamesema
documents zinaonyesha ilisajiliwa Tanzania.
Taarifa nyingine ya polisi imesema mzigo huo una thamani ya pound
millioni 50 ambayo kwa pesa za kitanzania ni kama 126,582,278,481 na
meli yenyewe ilikua na timu ya watu tisa ambao wanatoka Egypt na Syria
na mzigo wote wameupakia kutoka Uturuki.
Unaambiwa baada ya kuona mchezo wao umefahamika, watu waliokuwemo
kwenye meli waliamua kuanza kuichoma moto meli hiyo na wote tisa
walijirusha baharini kwa nia ya kutaka kukimbia lakini wakakamatwa
mapema tu na kukutwa na hizo dawa za kulevya aina ya hashish ambazo
thamani yake inagonga kwenye £50m.
Bandari husika ya Italia walipewa taarifa kwa siri mapema siku
kadhaa kwamba meli hii ilikua imebeba tani nyingi za dawa za kulevya
hivyo wakawa wanaifatilia kwa siku kadhaa kabla ya kuikamata.
Msemaji wa bandari amesema hawakutegemea kama meli hiyo ingekua
imebeba kiasi hicho cha dawa za kulevya na pia hawakutegemea kama watu
waliokuwemo ndani yake wangeichoma moto ili kupoteza ushahidi japo zoezi
hilo halikufanikiwa na dawa zikaonekana.
Meli hiyo imesogezwa kabisa mpaka kwenye bandari na moto umezimwa
huku msako zaidi ukiendelea kwenye sehemu nyingine za meli hiyo ili
kuona kama kuna dawa nyingine za kulevya huku watu wote tisa wakiwa
wanaendelea kuhojiwa.
HABARI HII Imetoka millardayo.com
No comments:
Post a Comment