Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Saturday, September 28, 2013

Hadji Adam, apata stashahada ya Sanaa ya maigizo leo toka chuo cha Bagamoyo,


Hongera Hadji Adam, apata stashahada ya Sanaa ya maigizo leo toka chuo cha Bagamoyo, ni mfano wa kuigwa
 (habri/picha na bongomovies)
Mwigizaji Hadji Adam leo amepata Stashahada yake ya maigizo ya drama na filamu toka chuo cha sanaa Bagamoyo mkoa wa pwani.
Katika mahafali hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa chuo hicho Hadji pamoja na wahitimu wengine wamepata zawadi na vyeti mbalimbali toka kwa uongozi wa chuo hicho.
Akizungumza na simu tokeo Bagamoyo alipo sasa Hadji amesema kuwa anajisikia furaha sana kuhitimu mafunzo yake yake hayo na anasema kuwa hapo ni mwanzo tuu na anajiandaa tena ili aendelee na elimu zaidi.
“kwakweli nina furaha sana siku ya leo, namshukuru Mungu nimemaliza salama na natumai nikipumzika nitaendelea na masomo zaidi hapo mwakani” alisema Haji.
Bongomovies.com tunapenda kumpa pongezi za dhati haji kwa hatua hii na tunamtakia kila la kheri katika masomo yake yanayokuja.
TOA MAONI YAKO HAPA:

No comments:

Post a Comment