(Habari / Picha: Na Ripoti Filamucentral / FC)
MWIGIZAJI wa kike Bongo Fatuma Makame ‘Joanita’ anakuja na filamu
inayojulikana kwa jina la Haraka ya Ndoa, Joanita ni moja kati ya mazao
ya mtayarishaji na muongozaji wa kitambo Mussa Banzi msanii huyo ambaye
ni mahiri katika uigizaji anaamini kuwa moja ya sababu inayokwamisha
wasanii ni mfumo wa usambazaji kwa sasa anakuja na kampuni nyingine ya
usambazaji............“Mimi sipeleki filamu yangu sokoni kwa Wahindi, hii filamu ya tatu kucheza nikiwa chini ya kampuni hii, filamu ya kwanza ni Mr. Shakaza ambayo ilisambazwa na wananchi lakini baadaye tukasambaza kwa kampuni ya Hamadombe ikafanya vizuri, pia tumetoa filamu ya Nipo Huru ambayo nayo imefanya vizuri na sasa ndiyo tunataraji kuiachia ‘Haraka ya Ndoa’ alisema Joanita.
Kwa mujibu wa Joanita filamu hiyo ya Haraka ya Ndoa itaanza kuuzwa mtaani mwezi wa Septemba, washiriki wakuu katika filamu hiyo ni Fatuma Makame ‘Joanita’, Chid Belami ‘Chidi’, Gango Gango, na wasanii wengine wakali wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu Swahilihood, Joanita anasema kuwa filamu hiyo italeta mapinduzi kwa kuwa itamfikia kila mtu sehemu alipo usambazaji wake ni nyumba kwa nyumba .
TOA MAONI YAKO HAPA:
No comments:
Post a Comment