Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Monday, September 9, 2013

BEKI WA TIMU YA YANGA MBUYU TWITE AVAMIWA NA WEZI USIKU MNENE:

Na Joan Lema na Hans Mloli wa GPL: CHAMPIONI
 
BEKI wa Yanga, Mbuyu Twite (pichani), amevamiwa na wezi nyumbani kwake usiku mnene na kukombwa vitu vingi vya ndani.
Tukio hilo lilitokea nyumbani kwa beki huyo raia wa Rwanda maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia Jumamosi.
Taarifa zinasema kuwa, Twite hakuhudhuria mazoezi siku iliyofuata katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola jijini Dar kutokana na tatizo hilo.
Mchezaji mmoja wa Yanga ambaye hakutaka kutajwa jina, alisema ni kweli beki huyo ameibiwa vitu vya ndani, lakini akasisitiza kwamba hajui ni vitu gani na vina thamani ya kiasi gani.
Championi Jumatatu lilipomtafuta Twite kuzungumzia suala hilo alikiri kweli ameibiwa lakini
hakuwa tayari kuzungumza chochote zaidi, badala yake akamtaka mwandishi amfuate mazoezini leo Jumatatu ili amueleze kila kitu.
“Kweli nimeibiwa lakini sitaki kusema chochote kwa sababu suala hilo lipo kwa viongozi wangu, lakini njoo kesho (leo) mazoezini naweza kukueleza kila kitu,” alisema Twite.
Baadhi ya wachezaji wa Yanga wakizungumza na Championi Jumatatu, walisema wanahisi wezi hao wanaweza kuwa ni mashabiki wa Simba, kwani mtaa anaoishi beki huyo umejaa mashabiki wa timu hiyo.
“Ukizingatia Mbuyu alichukuliwa kutoka Simba na ni beki mmoja mzuri balaa, hivyo mashabiki wa Simba bado wana hasira naye,” alisema beki wa Yanga, Juma Abdul.
Taarifa zilizopatikana jana zinasema tayari suala hilo limeripotiwa polisi.

TOA MAONI YAKO HAPA:

No comments:

Post a Comment