Wasanii wa filamu leo walikuwa kwenye kikao maalum kwaajili ya kuendelea kujadilia masuala ambayo yameendelea kuikumba tasnia hiyo, katika kudai haki yao ya kumiliki kazi zao, na kuomba baadhi ya viongozi katika Bodi ya filamu Tanzania kuweza kuachia ngazi
kutokana na kuwa kikwazo katika kutafuta haki zao. Wasanii hao
walisisitiza kama hawatapata nafasi nzuri ya kuweza kukaa pamoja na
waziri na kumweleza mambo yao, basi wataanzaisha maandamano makubwa ya
nchi nzima kuhakikisha baadhi ya viongozi wa Bodi ya Filamu wakitoka.
Baadhi ya wasanii walitaka wasanii wenyewe kwa wenyewe kwanza lazima waadabishane ilikuweza kuonyesha kwamba ufuatiliaji wa mambo yao yanakuwa ya kiuhakika na wa kufuata sheria kama inavyotakiwa. Hata hivyo baadhi wengine walidai kwamba, wapo wenzao wamekuwa kikwazo kwa kutofika katika kikao hicho, na kusababisha kuzoletesha nguvu ya mapambano dhidi ya maadui zao.
No comments:
Post a Comment