Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Monday, May 7, 2012

Unajua kwanini Cloud 112, ameenda kuzindulia filamu ya TOBA Zanzibar

  Msanii wa filamu nchini Issa Mussa Cloud 112 akiungana na kampuni ya Cl & Cy Company tayari imeshakamilisha maandalizi yakeya mwisho katika kuizindua filamu yake ya TOBA. Akizungumzia filamu hiyo Cloud alisema ni filamu yake ya kwanza ambayo ameigiza ng’ambo kabisa ya mji  yaani katika kisiwa cha Kigomboni katika kitongoji cha Bamba Beach. Cloud alisema filamu hiyo itakuwa ya kwanza katika histori ya maisha yake kuizindulia katika mji ambao alizaliwa na kuja Dar es salaam kuja kutafuta maisha.  Alisema kutokana na hali hiyo na ndiyo maana ameamua kuizindua kwa heshima kubwa kwa kumuarika kiongozi mkubwa wa  Zanzibar makamu wa raisi wa kwanza Maalim Sefu Sharifu Hamadi.
Aidha alisema filamu hiyo amefanya kiingilio kidogo ili kila Mzazibar aweze kuja kuangalia filamu hiyo, na aweze kujifunza kutokana na kuporomoka kwa maadili katikakisiwa hicho.  Filamu hiyo alisema kwamba inamaadili sana ya kidini ingawa haijabagua dini yoyote kwa kuwa ni filamu inayoelezea maisha ya kila mmoja ambaye anapaswa kurudi kwenye njia iliyonyooka katika kumuelekea mungu wake.  “Ni filamu ambayo nimeigiza na watu wachache sana, ila ni filamu ambayo nimekuwa nikiiwaza kwa muda mrefu katikakuitengeneza” alisema.  Katika filamu hiyo aliwataja pia kuwepo kwa Chiki Mchome, Salma Salimi ‘Sundra’ ambaye ameigiza kama mkewe, Yusuph Embe Awadhi na wengine wengi.   Cloud 112 alisema ni filamu ambayo amelitumia jina la Nasir,akiigiza kama kijana mtukutu ambaye hasikiki wala aambiliki,lakini mwisho wa siku jambo linalomkuta analijutia sana.
Aidha alisema maisha ambayo ameigiza humu ndiyo watu wengi wanaishi kwa kujiona fahari duniani,kumbe wote tunapita katika njia moja ya kuelekea kwa mwenyezi mungu. Filamu hiyo itazinduliwa siku ya May 18 mwaka huu, katika Hotel ya Bwawani  kuanzia saa moja usiku , saa 3;00 ndipo uzinduzi kamili utafanyika. Kutakuwa na dufu pamoja na utizamaji wa Tv moja kwa moja ya filamu hiyo.  Wakati huo Cloud 112 hiyo ndiyo shukrani yake kwa Wazanzibar wenzake, maana alianza kama masihara  wakati huo yupo  Shule ya Msingi Darajani, Kisiwani Unguja Zanzibar. Anasema akiwa shuleni alichaguliwa kuwa miongoni mwa wanafunzi ambao walikuwa na kazi ya kutunga mashairi, na maigizo mafupi.   Aidha alisema maisha ambayo ameigiza humu ndiyo watu wengi wanaishi kwa kujiona fahari duniani,kumbe wote tunapita katika njia moja ya kuelekea kwa mwenyezi mungu. Filamu hiyo itazinduliwa siku ya May 18 mwaka huu, katika Hotel ya Bwawani  kuanzia saa moja usiku , saa 3;00 ndipo uzinduzi kamili utafanyika. Kutakuwa na dufu pamoja na utizamaji wa Tv moja kwa moja ya filamu hiyo.
Anasimulia zaidi akisema kipindi hicho Mwalimu wake Mkuu Mwajuma Sadat, alikuwa mtu wa kwanza kugundua kipaji chake na kumhamasisha na kumfundisha kutunga michezo ya kuigiza yenye kuvutia zaidi.   Anasema alimfundisha jinsi ya kutunga mashairi, pamoja na michezo ya jukwaani baada ya kugundua kuwa mwanafunzi wake (Cloud) alikuwa ni mwepesi sana kuelewa.   Baada ya kumaliza shule ya msingi Cloud alijiunga na Shule ya Sekondari ya Haile Selassie iliyopo pia kisiwani Zanzibar na akiwa sekondari, hakujihusisha tena na sanaa, bali alitilia mkazo elimu ingawa kwa bahati mbaya alishindwa kufanya vizuri kwenye mtihani wa kuingia Kidato cha Tano na kulazimika kurejea nyumbani.

Alipoanza maisha ya nyumbani alipata bahati ya kufanya kazi katika duka lililokuwa
likimilikiwa na Abdalah na mkewe Asia Kindi ambalo lilikuwa likiuza nguo kisiwani Zanzibar.
Anasema kipindi hicho nguo nyingi zilikuwa zikitoka Dubai, Oman na India na kuuzwa
Zanzibar. Hatua hiyo ilimlazimu , mara kwa mara kwenda nchi hizo kutafuta nguo kwa ajili ya biashara.
Nguo ambazo mara nyingi alikuwa akizifuata, na ndizo zilizokuwa na soko kubwa ni zile za akinamama na watoto.   Anasema mwaka 1992 alifanya safari yake ya kwanza kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya biashara na kurudi tena Zanzibar. Safari kati ya Zanzibar na Dar es Salaam ziliendelea hadi mwaka 1997 ambapo Cloud anasema alihamisha makazi yake rasmi kutoka Zanzibar hadi Dar es Salaam.  Akiwa jijini Dar es Salaam kaka yake aliyekuwa akiitwa Ali Rashid alimtafutia kazi kwenye Kampuni ya Alnaim Enterprises, katika Hospitali ya Al Ijumaa.   Anasema alifanya kazi hapo kwa muda wa miaka minne na mwaka 2001 akajiunga na kampuni mpya ambayo ilimwajiri kama msimamizi wa usiku katika Hoteli ya Sleep Inn katika maeneo ya Kariakoo, katika makutano ya mitaa ya Narung’ombe na Lumumba.

Ni wakati huo akiwa anafanya kazi katika hoteli hiyo, Cloud alipata muda na nafasi ya kuanza kufuatilia vipindi vya maigizo kupitia Kituo cha Televisheni cha CTN, hatua iliyomfanya kuanza kupata mawazo ya kurejea katika fani yake ya sanaa.   Anasema igizo ambalo kwa kipindi hicho alilifuatilia kwa kina ni igizo la Hasidi, ambalo   lilimvutia sana na kumpa shauku wa kujiunga na kundi hilo la sanaa ili awe muigizaji.
msanii huyo anasema kwa vile wakati ule kulianzishwa Chuo cha kujifunza kuigiza jijini Dar es Salaam cha Spleended aliamua kutumia fursa hiyo kujiunga na chuo hicho ili kukuza zaidi fani yake na kuibua mbinu mpya katika tasnia ya uigizaji. Nyota yake katika ugizaji ilianza kuonekana mwaka 2001, pale alipoigiza filamu ya kwanza iliyojulikana kwa jina la Emorata, iliyozungumzia masuala ya ukeketaji ikasambazwa na Mwananchi Store.

Filamu ya Emorata ilimtambulisha vizuri katika ulimwengu wa filamu akijulikana kama
Mjombamjomba, akiigiza kama mjomba wake Chekibudi. “Miezi michache baadaye
kuliandaliwa tamasha kubwa la mashindano ya jukwaani, kati ya Kaole Sanaa Group na
kundi letu la Spleended Sanaa Group.   Mwaka 2003 akiwa na kundi la Spleended, Cloud aling’ara tena pale walipoanza kurusha igizo la Kimbunga, na baadaye igizo hilo lilifuatiwa na igizo la Mtaji wa Maskini ambapo sasa alianza kutumia rasmi jina la Cloud. Akizungumzia chanzo cha jina Cloud anasema alibatizwa jina hilo miaka mingi iliyopita  wakati huo akiwa na kundi lake la kwanza katika uigizaji la New Generation lililokuwa Zanzibar.

Ni baada ya mafanikio yote hayo akiwa na makundi ya uigizaji hatua iliyomuwezesha kuwa msanii nyota, Cloud alichukuliwa na Kampuni ya GMC wakaandaa filamu iliyoitwa Sabrina, stori ikiwa imetungwa na George Tyson.   Kampuni hiyo ilikuwa inamilikiwa kwa pamoja kati ya Chekibudi na Dude. Katika filamu hiyo ilibidi Chekibudi aigize kama mhusika mkuu, na Cloud aigize kama daktari ambapo angeweza  kuonekana mara moja tu.   Hata hivyo Tyson alishauri na kumchagua Cloud kuwa mwigizaji mkuu na mume wa Vyonne  Cherry ‘Monalisa’ na Chekibudi kuwa daktari jambo analosema lilizua kasheshe. Anasema ilibidi Chekibudi atafakari suala hilo kwa muda wa karibu saa saba, hatmaye alikubali.   Katika Filamu ya Subrina Cloud alionesha uwezo wa hali ya juu, kutokana na kucheza kwa hisia kali na hatmaye wapenzi wengi wa tasnia ya filamu waliweza kubaini kipaji kilichopo ndani ya
msanii huyo.   Ni kutokana na mafanikio aliyoyapata kupitia filamu ya Sabrina , Cloud alianza kujipanga ili kutoa filamu yake mwenyewe iliyojulikana kama Security, ambayo aliigiza kati ya Zanzibar na Dar es Salaam.   Katika uigizaji wa filamu hiyo alishirikiana vilivyo na Cynthia ambaye kwa sasa ndiye mkewe na ameza naye mtoto mmoja ambaye anaitwa Nabil ‘Prince, Cloud Junior’ . Kukamilika kwa filamu ya Security iliyomchukua miaka miwili kuiandaa kutokana na ufinyu wa fedha kulimpa nafasi Cloud kuweza kuandaa filamu ya Valentine Day na kumuuzia Sara Mwakapala mwaka 2007.   Ndipo nilipozungumza na Steps Entertaiment na kuingia nao Mkataba wa filamu ya kwanza iliyokwenda kwa jina la Ukiwa, ambayo iliniwezesha kupata fursa ya kuongezewa Mkataba wa filamu nyingine sita.”
Filamu ambazo aliingia nao mkataba ni Basilisa, Kinyonga, Sulia, Tifu la Mwaka, Samanta,
Tripple L na filamu yenye mahadhi ya kidini ya Toba. Mwaka huu 2012, Cloud ameingia nao Mkataba mpya, ambazo zote anategemea kuzitengeneza kupitia Kampuni ya CL & Cy Company.   Kampuni hiyo ambayo inajihusha na kuandika stori akishirikiana na Cynthia, Mc, hujishughulisha na uhariri wa video na udalali wa magari. Alisema maendeleo makubwa aliyoyapata katika filamu ni kutoka katika hali ya utegemezi na kuwa mtu anayejitegemea, kuwa na kampuni yake ambayo imesajiliwa na kuwa na jina kubwa.   Tuzo alizopata ni mwongozaji bora wa filamu mwaka 2012, iliyotolewa na Mini Ziff Red Capert jijini Dar es Salaam, pia alipata tuzo ya mwigizaji aliyoiletea maendeleo Steps Entertaiment. Ameshapata mialiko mbalimbali ya kucheza filamu za nje, ikiwemo moja aliyoicheza na Wamarekani.

“Kitu ninachokichukia ni kumuona mtu anadharau kazi yangu ya uigizaji wa filamu hasa wale ambao tunapoahidiana wao wanachelewa kwenye shooting, na wengine kuomba nafasi zao waigize haraka na kuondoka wakati wamepewa fedha nyingi.”

Zifuatazo ni picha zaidi za filamu hiyoo... Please!! Usiiikose.





Baada ya maovu kumzidi alikwenda kutupwa kwenye moto

Mambo kwa Nasir 'Cloud 112' yalizidi kwenda vibaya kwani alijaribu kujitetea lakini ilishindikana.




No comments:

Post a Comment