Lile
nguli la filamu za kuchekesha Tanzania, Athuman
Majuto ‘ King Majuto’, hivi karibuni aliingia mkataba na wauzaji wa
bidhaa za Azam, na kumchukuwa akiwa kama Balozi mpya wa bidhaa hizo huku
akishirikiana na Hussein Kiety 'Sharo milionea' katika kazi zake.
Majuto alisema mkataba na kampuni ya Al – riyami ameuvunja kwa kuwalipa
shilingi milioni 20. Alisema kampuni ya Al - riyami kwa sasa imekuwa
inarusha kipindi cha
Vituko Show zile ambazo aliigiza zamani wakati yupo nao.
“Sasa hivi
kazi zote nitakuwa nikizifanya kwaajili ya bidhaa za Azam, pia nipo kwenye
mikakati mingi juu ya kazi zangu mpya” alisema.
Hata
hivyo
King Majuto kwa sasa kazi zake atakuwa akifanya Dar es salaam na
akimaliza
anarudi Tanga ambapo kazi zake zingine zinaendelea, wakati huo huo
katika kampuni hiyo anaenda kukutana na mzee Small ambaye amekuwa
akitangaza bidhaa za kampuni ya Azam kama vile tui la nazi katika bidhaa
ya Azam.
|
blog yako iko poa sana Cloud
ReplyDeletejacque belgique