Msanii wa muziki wa kizazi kipya Cpwaa amesema kutengeneza video za
gharama kwaajili ya kujitangaza katika soko la kimataifa zaidi na wala
aangalii maslahi ambayo anayapata kutokana na kazi hiyo. Cpwaa alisema
kama video yake mpya ya Mhhh, ambayo kwa sasa inatamba sana katika vituo
mbalimbali vya Tv alitumia dola elfu 10 sawa na milion 1.5 kwa sasa, hii ni kutokana na kusafiri na watu
wanne usafari wa ndege wa kwenda na kurudi Afrika Kusini pamoja na
kulala katika Hoteli ambayo pia waliifanyia video hiyo, kuwalipa Mamodal
na kukodi vifaa kwaajili ya kuchukulia video. Alisema kwamba watu
alioondoka nao hapa ni Meneja wake ambaye ni Mzungu, Producer wa video
Adam Juma wa Next Level pamoja na Produce r wa wimbo huo Luk. |
No comments:
Post a Comment