Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Tuesday, May 1, 2012

Avengers itafanya Biashara kubwa zaidi - Robert Downey, Jr.



Robert Downey, Jr. au ukipenda muite Mzee wa Iron (Amecheza Filamu ya IRON MAN) amesema anategemea filamu mpya inayoandaliwa na Marvels iitwayo Avengers yakuwa itabamba ile kinoma ikiwa na pamoja kufanikiwa katika Tasnia ya Filamu Duniani kote kutokana na kuwa na Vipaji tofauti katika filamu hiyo.
Filamu hiyo imeshirikisha nyota mbalimbali na Majina yao toka Filamu ambazo wametamba nazo  ikiwa ni pamoja na Iron Man, The Incredible Hulk, Thor, Captain America, Hawkeye na Black Widow kimajina halisi ni Robert Downey, Chris Evans, Chris Hemsworth, Scarlet Johansson, Jeremy Renner, Mark Ruffalo na Mzee mzima Samuel L. Jackson.
Filamu inakisiwa kutumia kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 135 ambayo ni sawa na Bilion 205 za kitanzania (Mhhhh Kibongo bongo tunaweza toana damu namna hii).

 Pia aliiambia NewsBeat kuhusiana na Ulinzi na usiri uliowekwa juu ya mavazi yaliyotumika katika kushutia filamu hiyo hivyo hakuna ambaye atakayejua ni aina gani ya mavazi watakayokuja nayo na inabaki ni siri ya wahusika tu.
Filamu hii ya Avenger inatarajiwa kuingizwa Theatre Tarehe 4 mwezi huu wa tano kwa ajili ya matayarisho na kuingizwa sokoni.
Unaweza angalia Trailer yake jinsi ilivyo

na hii ndo Poster yake
Haya kwa wale wapenzi na wadau wa filamu tuisubirie kwa hamu filamu hii kwani Mastaa walioshirikishwa na kuchezeshwa humu ni balaa.

No comments:

Post a Comment