Basi la
kampuni ya Muro Investment,
T820BEY lillilokuwa likitokea Mwanza kwenda jijini Dar es Salaam, limewaka
moto na kuteketea kabisa maeneo ya
Maseyu Mkoani Morogoro. Ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 1:15 usiku Mei
8,2012, haikusababisha madhara kwa abiria isipokuwa mali zao zote ziliteketea
kwa moto
Mmoja wa wahusika wa basi hilo alidai kuwa
chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu ya umeme iliyolitokea gari hilo.
Inadaiwa kuwa gari hilo lilipata hitilafu katika taa na walipofika mjini
Morogoro walifanyia marekebisho na kuendelea na safari, walipofika maeneo
hayo ya Maseyu likashika moto.
Hata hivyo gari hilo liliteketea kabisa kwani hakukua na zima moto wala msaada wowote wa kuliokoa
No comments:
Post a Comment