Mwigizaji wa filamu nchini Stiven Nyerere akishirikiana na Steps Entertaiment wameizindua filamu ya Mwalimu
Nyerere kwa njia ya kutoa msaada katika kituo cha Maunga, kilichopo
Ananasif Kinondoni jijini Dar es salaam ilikuenzi jina hilo. Stive alisema
kufanya hivyo ni kama njia ya kumuenzi baba wa Taifa hili, kwani yeye
alikuwa akipenda sana watu jambo ambalo anaamini hata yeye akifanya
hivyo ni zawadi kubwa wa muasisi huyo. Stiven anasema alipofika Butiama
kwa mwalimu, alikuta watu wengi wakiwa na hamu ya kumuona mtu ambaye
anaitwa Stive Nyerere jambo ambalo walifurahi sana kumuona. Filamu ya
Mwalimu Nyerere inatarajia kuingia sokoni na kampuni ya Steps
Entertaiment siku ya ijumaa ya tarehe 26 May. |
No comments:
Post a Comment