Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Tuesday, May 8, 2012

Mkapa apanda kizimbani kutoa ushahidi dhidi ya mahalu

 RAIS MSTAAFU wa Awamu ya Tatu, Benjamin Willium Mkapa jana alipanda kizimbani kutoa ushahidi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Balozi wa zamani wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu

Katika kesi hiyo Profesa Mahalu na mwenzake, Grace Martin aliyekuwa Ofisa Utawala wa Ubalozi huo, walishitakiwa katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu kwa kuisababishia Serikali hasara ya Euro 2,065,827.60, kupitia mchakato wa ununuzi wa jengo la Ubalozi wa Tanzania Italia.

Mkapa alipanda kutoa ushahidi kwa kuwa wakati wa ununuzi wa jengo hilo yeye ndiye alikuwa Rais

Katika ushahidi wake Mkapa alionekana dhahidi shahiri kumtetea Balozi huyo, na kuiambia Mahakama kuwa anatambua mchakato mzima wa ununuzi wa jingo hilo na yeye ndiye aliyetoa idhini ya ununuzi huo na kusema mchakato wote ulikwenda vizuri.

Kesi hiyo iko mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Ilvin Mugeta
Katika ushahidi wake Mkapa alidai kuwa, Serikali yake ilifahamu ununuzi na alishangazwa kwa kushitakiwa kwa Mahalu

Akifafanua kuwepo kwa mikataba miwili katika ununuzi wa jengo hilo alisema malipo yalifanyika katika akaunti mbili tofauti

Alidai katika mchakato huo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wizara ya Ujenzi na Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi zote zilituma wataalamu wake kufanya tathmini ya jengo hilo kabla ya ununuzina hilo linajulikana nan hajawahi kupata malalamiko yoyote kutoka Itali.

Mkapa aliyeonekana kuongea kwa kujiamini huku akiwa wakati mwingine alishindwa kuzuia tabasamu alitoa ushahidi huo na kuainisha mengi mengineyio kuhusiana na ukweli alioujua

No comments:

Post a Comment