Shirikisho la wasanii Tanzania 'TAFF' leo limefanya kikao ili kuweza
kuangalia ni jinsi gani wanaweza kuendesha shirikisho hilo, kutokana na
upungufu wa fedha walizokuwa nazo. Raisi wa shirikisho hilo Simon
Mwakifamba, alisema shirikisho hilo halitegemei fedha kutoka Serikalini
hivyo ni juhudi zao pekee ndizo zinazoweza kufanikisha kwao. Alisema pia
sheria mbalimbali zimekuwa zikiwabana, hivyo huu ni wakati wa wao
kuungana na kushikamana ili kuweza kupamba juu ya ufisadi wanaofanyiwa,
kwenye tasnia yao kuanzia kwenye sheria ambao inawapa nafasi kubwa
Wasambazaji kuwa na haki.
Pia aliwataka wasanii kugangamala na kuungana pamoja ili kudai haki zao, katika kikao kilichofanyika Vijana, Kinondoni.Baadhi ya wasanii wakiwa kwenye kikao
Mkono na mwenzake, wakisikiliza kikao kutoka Al Riyam Production.
Dr Cheni akiwa na Dino
Steve nyerere akisikiliza mkutano
Jack Wolper akiwa na wasanii wengine wakishikana mikono kuashirikia mshikamano
No comments:
Post a Comment