Mkali wa muziki wa Hip Hop nchini Farid Kubanda 'Fid Q' ametukiwa na cheti na afisa mtendaji mkuu wa taasisi ya Under the Same Sun, Mr Peter Ash kutokana na kujitolea katika mapambano dhidi ya unyanyasaji wa walemavu wa ngozi na kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na walemavu wa ngozi ambao wanajulikana zaidi kama Albino.
Fid Q anasema Mr Peter ambaye pia ni mzungu albino alimtunukia cheti hivyo cha CERTIFICATE OF APPRECIATION, kutokana na kulidhishwa na mapambano na elimu aliyoitoa kwa jamii kuhusiana na ulemavu wa ngozi.
Alisema mapambano hayo yalikuwa zaidi katika mikoa ya kanda ya ziwa. Pia alisema ataendelea kutoa elimu kwa jamii na kuwaelimisha kwamba jambo hilo linaweza kutokea kwa jamii yoyote.
No comments:
Post a Comment