Mh. Ramadhan abdalla shaaban na Bw.Alex Knospe |
Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kampuni ya Royal Dutch Shell plc (shell) kwa pamoja wametangaza uwekaji saini wa Waraka wa Makubaliano.
Waraka huo unaweka bayana ushirikiano kati ya Kampuni ya Shell na Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar katiaka secta ya Mafuta na Gesi na inafafanua hususani kuhusu hatua za awali zinazohusiana na kujenga uwezo katika secta ya mafuta na gesi pamoja na maendeleo ya vijana katika kukuza ujuzi wao kwenye secta hii, ikiwa ni pamoja najitihada za elimu na uwezo wa ujasiria mali.
Axel Knospe, mwenyekiti wa shell deepwater Tanzania alieleza kuwa, kampuni ya shell ina nia ya kuwa na uhusiano imara na serikali ya zanzibar na pale itakapofaa, itaanza hatua za utafiti amabao utafanyika kwa njia endelevu,ya kiuchumi, kijamii na inayowajibika kimazingira.
Kwa upande wake wazir wa Ardhi,Nyumba, Nishati wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Mh. Ramadhani Abdalla Shaaban alisema kuwa utiaji saini wa waraka huo ni hatua kubwa inaoyoonesha jitihada za serikali za kuendeleza secta ya Nishati Zanzibar.
TOA MAONI YAKO HAPA:
No comments:
Post a Comment