FASHA JOSHUA
Mwanamuziki aliyekuwa Dubai Fasha Joshua amerudi upya katika bendi yake ya Twanga Pepeta, ilikuziba nafasi iliyoachwa na mwanadada ambaye alikuwa mnenguaji wa kundi hilo Lilian Internet, ambaye kwa sasa ameamua kuhamisha makazi yake hadi Mashujaa kwa kina Chaz Baba.
Kiongozi wa kundi la Twanga amesema amepokea taarifa za kuhama kwa mnenguaji wake huyo, lakini kwao haikuzuru kwakuwa tayari wanaye mnenguaji mwingine ambaye alikuwa likizo Uarabuni.
Wanenguji wa Twanga Kazini
Twanga Pepeta
Uongozi wa Twanga wamesema mnenguaji wao ameanza kazi rasmi jumatano hii, hivyo taratibu kazi zake zitaanza kuwa wazi mbele ya mashabiki wake.
Haya kwa wale ambao ni wapenzi wa Twanga kazi hailali mambo ni bandika bandua na kata funua, kazi kwenu.....
HALUUUUAAAAAAA!
No comments:
Post a Comment