Huyu mutu anaitwa Robin Van Persie au RvP au Van Penga kama alivyozoeleka, Siku ya leo (Jumamosi) ameendeleza kuonesha Cheche zake katika Ligi kuu ya Uingereza baada ya Kutupia Mawili peke yake na kuipa ushindi Arsenal wa magoli 2 - 1 dhidi ya Liverpool ambao walionekana kuutawala zaidi mchezo na kupewa kipaumbele kutoka kifua Mbele katika Mchezo huo.
Liverpool walikuwa wa kwanza kupata Goli kupitia kwa Laurent Koscielny ambaye alijifunga alipokuwa na hekaheka ya kuondoa mpira wa hatari uliopigwa toka wingi ya kulia na kuujaza kimiani.
RvP alisema hapana hiyo haiwezekani alikuwa kama mtu ambaye hayupo kabisa uwanjani lakini Ndizi iliyopigwa na Bakary Sagna toka wingi ya kulia ilimfanya van Penga Kuchomoka na kupiga kichwa matata kilichomuacha Pepe Reina hajui nini la kufanya
Hadi mapunziko Timu zote zilikuwa sare ya 1 - 1.
Kipindi cha pili Arsenal walionekana kuzidiwa zaidi lakini walikuwa makini sana kuondoa mipira yote hatari iliyoelekea langoni mwao.
Van Penga aliona haitoshi kuwa sare, katika dakika za Lala salama Alexandre Song alimtafuta Van Persie Yupo wapi na kumpatia Pasi matata ya kumchotea na Van Persie aliionganisha moja kwa moja bila ya hata kuiacha ipoe na Kumuacha Pepe Reina katika Mataa hajui nini la kufanya tena.
Kwa hali na Moto anaouwasha huyu mtu anaonekana kusumbua sana vilabu vya ulaya Mpaka kufikia Hatua ya Timu mbalimbali kubwa kuanza kumnyemelea ili kumsajili katika majira ya Joto (Dirisha Kubwa la Usajili) aisee the Man he's VANTASTIC
Wakati Huo huo,
Kocha Mkuu wa Kilabu cha Chelsea ya Uingereza ya Kaskazini Andre Vilas Boas (AVB) ameendelea kuwa katika wakati mgumu na Bosi wa timu hiyo baada ya timu yake Kupachikwa bao Moja kutoka kwa wenyeji wao West Bromwich Albion Bao lililowekwa kimianin na MacAuley na kuifanya Timu hiyo kupoteza point tatu muhimu na kuzidi kupunguza matumaini ya kuingia katika kundi la Timu Nne bora Uingereza (The Big 4). matokeo ambayo Mimi kama Injini ya jiji yamenisononesha kwa kweli, lakini naamini Tutajipanga vizuri na kurudi katika Fomu yetu kama hapo awali.
No comments:
Post a Comment