ZIARA ya kusaka vijana watakaoshiriki katika shindano la
Epiq Bongo Star Search mwaka huu inaanzia mkoani Dodoma Juni 15 katika Ukumbi
wa Royal Village.
Akizungumzia ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Benchmark Production Ritha Paulsen
alisema kuwa washiriki wanatakiwa kufika katika ukumbi huo kuanzia saa 12
asubuhi.
Alisema kuwa kampuni yake inatarajia kuchukua vijana watatu hadi
watano kutoka mkoa huo watakaouwakilisha mkoa huo katika fainali
zitakazofanyikia Dar es salaam.
Alisema kuwa wakiwa
mkoani humo wanatarajia kuona vipaji vya wasanii wa kila aina kwa kuwa EBSS
inalenga kukuza vipaji vya vijana wenye uwezo wa kuimba aina zote za nyimbo.
“ Kama ambavyo imeshafahamika kuwa mwaka huu mshindi wa EBSS
atapata kitita cha shilingi milioni 50 taslim hivyo ni kwamba tunawaomba wakazi
wa mkoa wa Dodoma
wenye vipaji kuja kwa wingi siku hiyo” alisema Ritha
Ritha ataongozana na majaji wengine ambao ni Salama na
Master Jay. EBSS mwaka huu imedhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya
Zantel.
|
No comments:
Post a Comment