Wanazmuziki
ambao wanaunda kundi la Offside Trick, mmoja wapo ameamua kujitoa na
inasadikiwa kwamba ameachana kabisa na masula ya muziki. Kiongozi wa
kundi hilo lenye makazi yake Zanzibar ila kwa sasa wamehamia Kigamboni
jijini Dar es salaam, ambao maarufu kwa kwa kupiga muziki wa mduala,
ambalo linatamba na nyimbo kama Dege, Bata, na Hammada, amesema kwamba
mwenzake kwa sasa yupo Zanzibar anaendelea na kazi zingine. Anasema
msanii mwenzake ambaye amejitoa ni Mudatiri
Masudi ‘Mudi Chriss’. lakini amesema baada ya kuondoka kwa Mudi Chriss
kwa sasa nafasi yake imechukuliwa na mwanamuziki kutoka pande za
hukohuko, Hammer Q,ambaye naye alishavuma na nyimbo za taarabu kama
vilePembe la Ng'ombe. (Picha ya juu ni Lil Ghetto na Hammer Q) |
No comments:
Post a Comment