HELLEN
DAVID (Candy) ambaye alikuwa miongoni kwa washiriki katika kinyang`anyiro cha
kumsaka mshindi wa “Tikisa 2011” na kutolewa katika hatua za mwisho za shindano
lile, ameachia Track yake mpya inayoitwa “NIMPENDE MILELE” chini ya kampuni
yaMost Record&Production ya jijini
dares salaam. Hellen au kwa jina la
kisanii anaitwa
California” ni
msanii ambaye anavipaji vingi, licha ya uwezo wake mkubwa wa kucheza muziki wa
kila aina pia ana uwezo mkubwa sana wa kuimba. Most Record & Production waliona
kipaji chake ndipo hawakusita kumpa ofa ya kurekodi nyimbo pamoja na video.
Baada ya ofa
hii aliyopewa na MostRecord &
Production, "Candy California”amepata ofa nyingine ya kurekodi nchini Afrika ya Kusini mapema mwezi
Juni 2012, ataweka wazi pale mipango yote itakapokuwa sawa.
Naitwa Issa Mussa 'Cloud112' karibu kwenye blog yangu, ambayo nitakuwa nikikuleteeni stori mbalimbali zikiwemo za filamu zangu zinazokuja na zilizopita, na za watu wengine karibuni sana.
No comments:
Post a Comment