Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Sunday, May 27, 2012

Sajenti asherekea siku ya kuzaliwa kwake

Mwigizaji wa filamu pia alikuwa Kimwana Manywele wa Twanga Pepeta Sajenti, juzi 25 May amejikuta akiwa mpweke baada ya kusherekea siku ya kuzaliwa kwake bila ya kuwepo kwa wasanii wa Bongo Movie na wa bendi ambao aliwatarajia kwa kuwapigia simu kwa muda mrefu, ambao aliamini wangekuja kumuunga mkono katika shehe hiyo. Hata hivyo majilani zake walikuja kwa wingi, na huku dada yake mpendwa akimpa mchango wa Dola mia moja katika koponi aliyoitwa.








 
 
 




 


Mambo yaharibika Zanzibar

Hali imezidi kuwa tete Zanzibar baada ya waandamaji wa Kiislamu wa jumuiya ya Uamisho wa Mihadhara ya Kiislamu kisiwani Zanzibar (JUMKI0 kuandamana, na kufanya mji wa Zanzibar usiwe na amani. Hali hiyo imedhibitiwa na askari polisi ambao wamekuwa wakijaribu kuzuia vurugu hizo zisizidi zaidi ya hapo. Hata hivyo hali bado imekuwa ngumu, kiasi cha watu wengi kutotoka kwenye majumba yao kwa baadhi ya sehemu.

Friday, May 25, 2012

Familia yenye upendo wakisherekea pamoja siku ya kuzaliwa kwa Mrs Cloud 112

Familia ya Cloud 112 ilikuwa ikifurahia siku ya kuzaliwa kwa Mrs Cloud 112, ambaye aliifanyia maeneo ya nyumbani kwake anapoishi maeneo ya Mwananyamala. Cloud 112 aliisherekea siku yao akiwa na mwanaye mpendwa Prince Nabil 'Cloud junior' siku yaa tarehe 12 May, wakati huo Nabil alikuwa pia akitimiza miezi 2 na siku kadhaa.






Dogo Aslay kuachia video ya tatu

Mwanamuziki Aslay Sadiq maarufu kama Dogo Aslay anatarajia kuachia nyimbo yake ya tatu tangu alipoanza kuachia nyimbo ya kwanza Niwe nawe, Naenda kusem na sasa anakuja na Umbea umbea akiwa na Saidi Juma maarufu kama Chege Chigunda. alisema wimbo huo anatarajia utamrudisha tena kwenye chati, kwakuwa kazi yake ya Naenda kusema ilimtambulisha, ila hii inaweza kumweka juu zaidi. alisema video hiyo anatarajia kuaichia siku ya  jumanne, ambayo aliitengeneza chini ya studio ya Poteza Rec kwa Suresh 'Mr India' (Kwenye picha akiwa na Dogo Muu, ambaye anatarajia kuja na video ya Shahidi)

Dogo Muu akiwa na Aslay

Aslay dogo Muu na H  number

Stive Nyerere azindua kwa kupelekea msaada watoto yatima

Mwigizaji wa  filamu nchini Stiven Nyerere akishirikiana na Steps Entertaiment wameizindua filamu ya Mwalimu Nyerere kwa njia ya kutoa msaada katika kituo cha Maunga, kilichopo Ananasif Kinondoni jijini Dar es salaam ilikuenzi jina hilo. Stive alisema kufanya hivyo ni kama njia ya kumuenzi baba wa Taifa hili, kwani yeye alikuwa akipenda sana watu jambo ambalo anaamini hata yeye akifanya hivyo ni zawadi kubwa wa muasisi huyo. Stiven anasema alipofika Butiama kwa mwalimu, alikuta watu wengi wakiwa na hamu ya kumuona mtu ambaye anaitwa Stive Nyerere jambo ambalo walifurahi sana kumuona. Filamu ya Mwalimu Nyerere inatarajia kuingia sokoni na kampuni ya Steps Entertaiment siku ya ijumaa ya tarehe 26 May.






















bibi mwenye kituo, Bi Zainabu Bakari






Cpwaa alenga soko la nje

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Cpwaa amesema kutengeneza video za gharama kwaajili ya kujitangaza katika soko la kimataifa zaidi na wala aangalii maslahi ambayo anayapata kutokana na kazi hiyo. Cpwaa alisema kama video yake mpya ya Mhhh, ambayo kwa sasa inatamba sana katika vituo mbalimbali  vya Tv alitumia dola elfu 10 sawa na milion 1.5 kwa sasa, hii ni kutokana na kusafiri na watu wanne usafari wa ndege wa kwenda na kurudi Afrika Kusini  pamoja na kulala katika Hoteli ambayo pia waliifanyia video hiyo, kuwalipa Mamodal na kukodi vifaa kwaajili ya kuchukulia video. Alisema kwamba watu alioondoka nao hapa ni Meneja wake ambaye ni Mzungu,  Producer wa video Adam Juma wa Next Level pamoja na Produce r wa wimbo huo Luk.

Cpwaa akiwa amepozi kwenye gari maeneo ya Leaders club