Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Monday, July 23, 2012

Vikao vya harusi ya Mtitu vyaendelea

Mwigizaji wa filamu nchini William Mtitu yupo kwenye mikakati ya kufunga ndoa Septembe 8mwaka huu. Vikao vimeshaanza katika kurekebisha mambo ya harusi yake, ambayo mwenyekiti wa kikao cha harusi yake ni Jacob Stephan 'Jb'. William Mtitu amesema mwanamke anayetaka kumuoa ni yule yule mpenzi wake wa muda mrefu, ambaye hausiki katika masuala ya sanaa ya filamu. Pia wasanii hao wapo katika mikakati ya kujua harusi hiyo itaenda vipi, Mc atoke wapi na ukumbi maeneo gani na jinsi ya kuendesha shughuli nzima. Hata hivyo kikao hicho bado hakijaenda sawa, kwakuwa leo wasanii wengine wamegawanyika wengine wameenda ZIFF, na wengine wapo IRINGA, wakati Mtitu yupo Shooting.









Friday, July 13, 2012

Kigoma kuwaka moto Julai 17

Wanamuziki wa kizazi kipya ambao wanaunda kundi la Kigoma Stars, kutokana na wanamuziki hao wote kutokea Kigoma wanatarajia kufanya bonge la Tamasha siku ya tarehe 17 ya mwezi huu. Wasanii hao ambao tayari wameshatoa wimbo mmoja unaokwenda kwa jina la Leka dutigite. Wasanii hao ni Mwasiti, Linex, Baba Levo, Diamond Platinum, Ali Kiba, Ommy Dinpozi, Rechal na wengine wengi. Pia inasadikiwa kwamba katika tamasha hilo, pia ;litaudhuliwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh Zitto Kabwe.

Mwasiti


Baba Levo

Thursday, July 12, 2012

Ujio mpya wa OPG Majingx

TOKA PANDE ZA MBEZI BEACH YULE MSANII MACHACHALI AMBAYE ALISHAWAHI KUVUMA NA VIDEO KALI MWAKA JANA ILIYOKWENDA KWA JINA LA SINA JIWE ALIYEMSHILIKISHA LINEX NA QUICK ROCKER BAADA YA KIMYA KIREFU SASA AMEIBUKA NA NGOMA MPYA INAYOKWENDA KWA JINA LA "BURGER" ALIYEMSHIRIKISHA BECKA TITLE MTOTO WA B.O.B PANDE ZA KINO MZIGO UPO TAYARI NA UMETAYARISHWA NA PRODUCER R.NAME TUNAOMBA SAPORT ZENU

Monday, July 9, 2012

Mechi ya Hisani ya kuchangia madawati yawa balaa

Wanamuziki wa muziki wa bongo Fleva jana walijikuta wakikubali kipigo cha 1 - 0  kutoka kwa mahasimu wao Bongo Movies katika mechi ya hisani ya kuchangia ujenzi wa madawati. Pia kwa upande wa Wabunge wa Simba waliwakunguta Wabunge wa Yanga bao 3 - 2. Hata hivyo kipigo kikali kilikuwa kati ya Wema Sepetu na Jackline Wolper, ambapo hadi sasa watu mshindi wa kweli hajajulikana, wakti Kasema na Cheka wakiishia kutunushiana misuri katika ulingo. Pata picha zaidi

wasanii wa Bongo Movie wakiwa kambini

Stive nyerere akiwa kambini

Cloud 112 akiwa ametulia wakati wakiwa kambini

Wakati wasanii wa Bongo Movie wapo kambini ndipo wakakutana na Wabunge wa Simba, hapa Jb akisalimiana na mbunge wa Kinondoni Iddi Azan.


Halima Mdee akiwa kambini