Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Saturday, April 28, 2012

Pole Sajuki

Cy & Cl Company inayomilikiwa na Cloud 112 na Cynthia  tunatoa pole kwa msanii mwenzetu Juma Kilowoko  'Sajuki' na mkewe Wastara, kutokana na maradhi ambayo yamemkuba Sajuki. Sisi wasanii wa  filamu tunaungana na wasanii wenzetu na wadau wote kwa kumuombea apate nafuu na kurudi kwenye kazi kama zamani. Pia naomba wasanii wenzangu tushirikiane katika haliu hii ambayo imemkuta mwenzetu, kwa msaada na mawasilino juu ya kumsaidia sajuki, wasiliana na Wastara 0713 666 113 kwa njia ya Tigo pesa, na 050000003047 katika benki ya Akiba Commecial yenye jina la Wastara Juma Issa.

Friday, April 27, 2012

Benzarelly aja na kitu kipya

                                                        BENZARELLY (BABUKUTOKA PANDE ZA MBEZI BEACH (MAKONDE) JIJINI DAR ES SALAAM, MSANII CHIPUKIZI WA BONGO FLEVA ANAYESUMBUA KWENYE MITAA MINGI YA HUKU MBEZI BEACH PAMOJA NA VITONGOJI VYAKE  KAMA KAWE NA TEGETA AYEJULIKANA KWA JINA LA CHRISTIAN BENZARELLY (A.K.A BENZARELLY) AMEACHIA TRACK YAKE MPYA KABISA INAYOKWENDA KWA JINA LA "KONA ZOTE ZA DAR"   KAZI NZURI YA MKONO WA MTU MZIMA G5, PANDE ZILE ZA MBEZI BEACH DAR. BENZARELLY ANAWAAMBIA MASHABIKI WAKE WAKAE MKAO WA KULA KWANI YUPO MBIONI KUACHIA TRACK ZINGINE MFULULIZO AMBAZO ZITAKUJA KUMBAMBA ILE MBAYA...!
 BENZARELLY PROFILE:
 JINA LA MSANII :  CHRISTIAN  BENZARELLY (A.K.A BENZARELLY)
 JINA LA WIMBO : KONA ZOTE ZA DAR
 STUDIO            : DUBI RECORD
 PRODUCER
       : G5

Cloud 112 alazwa

Msanii maarufu wa filamu nchini Issa Mussa 'Cloud 112' amelazwa katika hospitali ya Al Ijumaa iliyopo Kariakoo baada ya kuugua ghafra, wakati akiwa katika shughuli zake za kawaida.  Cloud 112 amelazwa hospitalini hapo tangu saa saba mchana,na hivi sasa tayari ameshapata vipimo vya Malaria ambayo amekutwa hana, pia akapimwa na presha ambapo alikutwa ipo sawa, hali iliyopelekea kuchukua vipimo vya typhod. Hadi hivi sasa msanii huyo bado yupo hospitali kwaajili ya kuendelea kuangalia afya yake na kuchukuliwa vipimo zaidi, wakati huo pumzi ndiyo inayomsumbua kwa kuwa anaipata kwa tabu

hapa akiwa hospitali ametundikiwa dripu ya maji

Thursday, April 26, 2012

Linah aendeleakung'aa DC Washngton

Msanii wa  muziki wa kizazi kipya kutoka Nyumba ya Vipaji Tanzania THT , Linah Sanga, ameendelea kufanya vizuri katika tamasha lake ambalo anafanya katika Tour maalum ya TAMANI Tour huko Dc Washngton Marekani. Linah pia anawashukuru mashabiki wake kwa kumpigia kura katika tuzo zaKilimanjaroMusic Award ingawa alikosa tuzo hizo.


Ujumbe wa Ray kwa mashabiki wake

Yapata wiki tatu sasa tangu msanii mwenzangu Steven Kanumba aage dunia, na kama ilivyo kwa kila kitu kinapotokea huandamana na kila aina ya maneno na hisia mbali mbali kutokana na mitazamo ya watu kupishana kuhusiana na jambo husika. Kulingana na muktadha huo, msiba wa Steven Kanumba umekumbwa na maneno na hisia kama hizo, hususan mazingira ya kifo chake; kinachosikitisha zaidi watu wengi (ambao wanajitambulisha kama wapenzi wa Kanumba), na baadhi ya vyombo binafsi vya habari vimekuwa vikinihusisha na kifo hicho, kwa kusema kwamba kwa njia moja au nyingine ninahusika na mauaji ya Steven Kanumba. Kwa muda wote huo tangu msiba ulipotokea mpaka leo hii nashika kalamu kujaribu kuyaweka sawa na kuondosha hisia chafu katika fikra za watu, nimekuwa nikipitia katika wakati mgumu sana kwa jinsi ambavyo nimekuwa nikinyooshewa vidole kila upande nikihusishwa na kifo hicho, kiujumla nimezingatia maoni ya wapenzi ya mashabiki wangu wakinitaka kuwa na subira,  ila kuna ukweli usemao kwamba, uongo ukirudiwa sana jamii huusadiki na kuuona ukweli, nimeona nisikae kimya ila niweke sawa hili kwamba sihusiki na kifo cha Steven Kanumba.
Nasema wazi kwanza sihusiki kabisa na kifo cha Kanumba kwanza kwa kuzingatia mazingira yenyewe ya kifo kilivyotokea. Wakati kifo hicho kinatokea, nilikuwa sehemu nyingine kabisa na mimi nilikuwa mtu wa tatu kutaarifiwa kwamba Kanumba amepatwa na mkasa ambao baadae ulisababisha kifo chake. Na na hata nilipofika katika hospitali ya Muhimbili (tofauti na watu wanavyodhani kuwa nilifika nyumbani kwake; ukweli mimi nilimkuta tayari amepelekwa Muhimbili), nilikuta tayari alikuwa ameshafariki ndio maana hata Polisi wanaohusika na usalama wa raia, si tu kwamba hawakuniweka chini ya ulinzi, sikuitwa hata kuhojiwa kwa sababu hakuna mazingira yoyote yanayonihusisha mimi na kifo hicho.
Pili, watu wanahusisha tofauti za kibinadamu zilizokuwepo baina yetu na kifo hicho, nasema hii sio sahihi kwa sababu kwanza ni kawaida kwa binadamu kutofautiana, isipokuwa kwetu sisi baadhi ya vyombo vya habari vilikuwa vinakuza kwa sababu nisizozijua, hivyo jamii ikachukulia kuwa tofauti zile ni uadui kitu ambacho sio sahihi, kwani sisi hatukuwa watu pekee tunaotofautiana kwani huu ni mwenendo wa kawaida wa dunia; hivi jana tumeshuhudia Waziri mmoja akieleza bayana katika mkutano na waandishi wa habari kuwa na tofauti na naibu wake, lakini hatuajasikia ikiandikwa wana ‘bifu’ bali imetafutwa lugha nzuri ya kupamba tofauti hizo, kwa kuwa waliohusika ni waheshimiwa, ila kwa wengine kutokana na sababu tusizozijua, inaonekana kama ni haki yetu kuandikwa vibaya. Kinachosikitisha, kwa nini jambo hili linachukuliwa kwa mkazo mkubwa sana, kwani hatujawahi kusikia watu wakiwa wanatofautiana na ndugu jamaa hata na marafiki zao na inaonekana kawaida tu? Kwani vyombo vya habari havikuwahi kuandika kuwa marehemu Steven Kanumba alikuwa na tofauti na baba yake, na yeye mwenyewe alitamka hivyo katika vyombo vya habari, mbona wameliongea bila kuongeza chumvi, na jamii inaona kuwa ni jambo la kawaida la kibinadamu.
Pengine watu wanaojaribu kuongea hayo, hawajui mimi na Steven Kanumba tumetoka wapi? Sisi si watu tuliokutana barabarani, tuna historia katika kazi yetu ya sanaa na pia katika maisha maisha yetu. Mwanzoni kabisa, mimi ndiye niliyempokea Kanumba pale Kaole na ndiye niliyemfundisha sanaa pale (nadhani watu wanakumbuka tamthiliya za wakati huo ITV) na baada ya hapo tulienda pamoja katika kampuni ya Game 1st Quality pamoja na tukafanya filamu kama Johari, Sikitiko Langu, Dangerous Disire na nyinginezo, na tuliendelea kuwa pamoja katika kampuni hiyo mpaka tulipofanya filamu ya Oprah mwaka 2008 ambapo niliingia rasmi kufanya kazi za kampuni yangu, lakini tuliendelea kuwa pamoja hata wakati nikiendelea na kazi za kampuni yangu. Pia mimi nilikuwa wa kwanza kuanza kufanya kazi na Steps na baadae Kanumba alipoanza kufanya kazi zake mwenyewe na kunikuta huko tuliendelea kuwa pamoja kama siku zote. Kitu kikubwa kilichokuwa kinaendelea baina yetu, ni kwamba tulijenga ushindani wa kuendeleza kazi mbele kwa kila mmoja akitoa kazi, mwingine anamjibu,  Isitoshe hata vitu vyetu binafsi utaona kama kuna kufanana; kuna wakati Kanumba alinunua Toyota Ruv 4 nyeusi mimi nikanunua ya kijani, aliponunua Harrier na mimi nikanunua pia, na hata gari za hivi karibuni, ukitazama utaona kuwa zinafana kwa karibu; hii ilikuwa ni kama maisha yetu, hatukuwa na uadui, ilikuwa tunapeana changamoto za maendeleo.
 Watu wanaojaribu kuonesha kuwa tofauti zetu ilikuwa ni uadui, huwa hawajui wapi tulikotoka ndio maana wanasema wasemavyo na katika kuthibitisha kuwa tofauti hizo hazikufikia katika uadui, kuna watu ambao wanafanya kazi nami katika kampuni yangu ya RJ ndio hao hao Kanumba alikuwa anawatumia siku zote katika kazi zake, hata baada ya tofauti hizo hakuna aliyekoma kufanya kazi na yeyote kati yetu. Hii inathibitisha kuwa tofauti ilikuwa kati yetu kama binadamu, sio chuki za kimafanikio, ingekuwa hivyo watu kama Junior Syaary ambaye mara nyingi hufanya final editing katika RJ ndio huyo huyo alikuwa akifanya na Kanumba, Ally Yakuti ambaye anaandika script za RJ, ndiye huyo huyo aliyekuwa anaandika kwa Kanumba, Steven Shoo ambaye ni mtaalamu wangu wa light, ndiye huyo huyo anayetumiwa na Kanumba na wengine wengi kama Juma Chikoka aliyecheza kikamilifu katika filamu ya kijiji cha Tambua Haki, ambaye pia anashiriki filamu nyingi za RJ, na wote hao, hawakuanzia kwa Kanumba, wote wameanza kwangu mimi ndio niliompatia na hata baada ya hayo yanayosemwa kuwa kuwa ni uadui, sikuwahi kuwakataza kufanya kazi na Kanumba.
Tatu kumtuhumu mtu kwa namna yoyote ile bila ya uthibitisho wa tuhuma hizo, ni kosa kwa sheria za nchi na pia kama ni mfuasi wa dini yoyote ni dhambi, kwani wakati ukisema hayo huku hujui uhalisia bali unasukumwa na nguvu za hisia tu ni sawa na kumchafua mtu huyo katika jamii bila ya kujua jamii inamchukuliaje. Napenda kusema wazi wazi kuwa, kwa kila anayetekwa na wimbi hili, ajaribu kufikiria leo ipo kwangu mimi, kesho inaweza kuhamia kwako, kwani mimi sio wa kwanza kufikwa na haya, inaweza kukukuta hata wewe au ndugu yako, utajisikiaje. Na kama kweli mimi nimehusika na kifo cha Kanumba kwa namna yoyote ile, basi Mungu atanihukumu na kila aliye hai atashuhudia, ila kama sijahusika kwa lolote, Mungu hatonihukumu na badala yake ataniinua, kwa kuwa ninapita katika kipindi kigumu mno sasa hivi kwa madhila haya.
Mwisho kabisa napenda kumaliza kwa msemo usemao, ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke, kwani kadri mambo haya yanavyoendelea, usidhani yataishia kwangu, kwani mkono wa dhuluma haushii karibu, ukisikia jirani anapiga kelele za mwizi, usilale kamsaidie, usiseme kuwa hatuhusiki kwani hayupo kwetu, kesho utafikwa na wewe utakosa wa kukusaidia. cha msingi kama tunampenda sana ndugu yetu ni kumuombea kwa Mungu, kwani hatujui makao yake huko aliko, na sio kuunda vitu ambavyo kamwe hata yeye angekuwa hai asingeviafiki.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU STEVEN KANUMBA MAHALI PEMA
 PEPONI
MUNGU IBARIKI AFRIKA MUNGU IBARIKI TANZANIA

Wednesday, April 25, 2012

Tmk, Shilole, Ferooz, Belly Black na wengine kuivamia Iringa na Songea

MENEJA wa kundi la Tmk Wanaume Family Saidi Fella, ameungana na  wasanii zaidi ya kumi na mbili katika sherehe ‘Party’  maalum siku ya burudani mkoa wa Iringa.
Saidi Fella  alisema, party hiyo itafanyika may 6  katika kiwanja cha Samora, baada ya kuombwa kufanya burudani na mashabiki baada ya kukaa muda mrefu bilayakufanya kufanya tamasha kwenye mkoa huo.
(Ferooz)
Alisema miongoni mwa wasanii ambao watakuwepo siku hiyo ni Feroozi Mrisho’Ferooz’, Zuwena Mohamedi ‘Shilole’, Berry Black, Nurudini ‘Baba Kitorondo’, Saidi Juma, ‘Chege’, Amani Temba ‘Muheshimiwa Temba, Aslay Sadiq ‘Dogo’ Aslay, Ize Man, Dogo Muu na wengine.
(Dogo Aslay)
Pia alisema hata hivyo ijumaa ya may 4 wanatarajia kundi hilo lote kufanya tamasha mkoani Songea katika ukumbi wa jambo Lee wakati mchana watakuwa kwenye viwanja vya Majimaji.
Shilole
Bibi Cheka atakuwemo

Cand aja na mapya kwenye muziki

HELLEN DAVID (Candy) ambaye alikuwa miongoni kwa washiriki katika kinyang`anyiro cha kumsaka mshindi wa “Tikisa 2011” na kutolewa katika hatua za mwisho za shindano lile, ameachia Track yake mpya inayoitwa “NIMPENDE MILELE” chini ya kampuni ya  Most Record&Production ya jijini dar  es salaam. Hellen au kwa jina la kisanii anaitwa
California” ni msanii ambaye anavipaji vingi, licha ya uwezo wake mkubwa wa kucheza muziki wa kila aina pia ana uwezo mkubwa sana wa kuimba. Most Record & Production waliona kipaji chake ndipo hawakusita kumpa ofa ya kurekodi nyimbo pamoja na video.

Baada ya ofa hii aliyopewa na Most  Record & Production, "Candy California”  amepata ofa nyingine ya kurekodi nchini Afrika ya Kusini mapema mwezi Juni 2012, ataweka wazi pale mipango yote itakapokuwa sawa.





Thursday, April 19, 2012

Hammer Q aziba pengo la MudiChriss Offside Trick

Wanazmuziki ambao wanaunda kundi la Offside Trick, mmoja wapo ameamua kujitoa na inasadikiwa kwamba ameachana kabisa na masula ya muziki. Kiongozi wa kundi hilo lenye makazi yake Zanzibar ila kwa sasa wamehamia Kigamboni jijini Dar es salaam, ambao maarufu kwa  kwa kupiga muziki wa mduala, ambalo linatamba na nyimbo kama Dege, Bata, na Hammada, amesema kwamba mwenzake kwa sasa yupo Zanzibar anaendelea na kazi zingine. Anasema msanii mwenzake ambaye amejitoa ni Mudatiri Masudi ‘Mudi Chriss’. lakini amesema baada ya kuondoka kwa Mudi Chriss kwa sasa nafasi yake imechukuliwa na mwanamuziki kutoka pande za hukohuko, Hammer Q,ambaye naye alishavuma na nyimbo za taarabu kama vilePembe la Ng'ombe. (Picha ya juu ni Lil Ghetto na Hammer Q)

Mudi Chriss aliyejitoa Offside Trick

Kundi la Offside Trick, mwanzo kabla ya kujitoammoja wapo.

Drogba ni nomaaaaaaa!

Nyota wa Chalsea Didier Drogba jana aliwainua kimasomaso mashabiki wa Chalsea kwa kutikisa nyavu za wapinzani wao Barcelona katika mechi ya kuwania kuingia nusu fainali. Drogba hakucheza makosa kwenye kipindi cha kwanza, na hatmaye aliandikia bao la kwanza na la mwisho timu yake.

Wednesday, April 18, 2012

HONGERA CHELSEA SAFI SANA

                                          Tujipongezee sana                                  

Video mpya ya Amini

Mwanamuziki wa kizazi kipya Amini Mwinyimkuu, ameshakamilisha video ya wimbo wake mpya ya Niwewe, na kusema picha zilizokuwemo kwenye video hiyo ndizo watu walizozitumia na kusema kwamba ameoa. Mwanamuziki huyo anasema yeye hakuoa, na picha zilizotumika humo ni za video ya wimbo huu. 



Zola na Mb Dog waliendeleza Burudani German

Mwanamuziki Zola D na Mb Dog  bado wapo Ujerumani katika jiji la Munich, katika show zao za bara la Ulaya. Zola D anasema anashukuru  sana mashabiki wao, kwani wamekuwa wakiitia wimbo wao na kujaa katika Show zao bila ya kutegemea. Wanasema huvi sasa bado wanaendelea katika miji mbalimbali ya nchi ya Ujerumani, kabla ya kuelekea Denmack na nchi zingine za Ulaya

Mb Dog akiimba wimbo wa Ratifa, huku wazungu kwa waswahili wakicheza.


Zola D na Tinah wanaounda kampuni ya Tizo Entertainment Ltd