Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Showing posts with label GOSSIP NEWS. Show all posts
Showing posts with label GOSSIP NEWS. Show all posts

Monday, November 4, 2013

SHAROBARO ALA KICHAPO KISA MKE WA MTU


 Kwa vile mke wa mtu sumu nimeona ni bora ni share na nyinyi watu wangu hii habri isome kwa kituo
 Issa Mnally Na Richard Bukos(gpl)
KIJANA mmoja mtanashati ‘Sharobaro’ ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja juzikati alijikuta akichezea kichapo cha mbwa mwizi kisa kikidaiwa kuwa ni mke wa mtu.

Usione vyaelea: Sharobaro (katikati) akilia baada ya kuchezea kichapo kwa kukutwa na mke wa mtu.
Tukio hilo lilijiri saa saba usiku mwishoni mwa wiki iliyopita, Chalinze mkoani Pwani ambapo mapaparazi wetu walikwenda kwa ajili ya uzinduzi wa kundi jipya la sanaa liitwalo 3 Ways.
Wakati shamrashamra zikiendelea, ghafla liliibuka timbwili na katika kufuatilia ilibainika sharobaro anayeishi eneo hilo alikuwa

Tuesday, October 29, 2013

RATIBA YA MAZISHI YA MAREHEMU MZEE SEPETU NILIYOIPATA:

RAY:
Habari zenu ndugu zangu, i hope mmeamka salaama salamin, kwa wale wagongwa allah atawaafu inshaallah:
Tangu juzi nimekua nikishare na nyinyi taarifa za Msiba wa Baba Mzazi wa Mwanafilamu mwenzangu WEMA SEPETU mzee ABRAHAM SEPETU:
Taarifa hizi nazipata kutoka kwa Ndugi wa Karibu wa Wema Sepetu ambae ni Binamu yake anaeitwa RAY ambaye ni Mkurugenzi wa Bendi ya Cococnut Zanzibar;
Ratiba YA Mazishi yatakavyo kua Kisiwan Zanzibar:
PICHA YA MAREHEMU ABRAHAM SEPETU ENZI ZA UHAI WAKE:
''Maiti itaondoka na Boti ya Kesho Asubuhi kuelekea Zanzibar na Kufikishwa Moja kwa moja kanisani kwa misa fupi kisha baraza la wawakilishi la Zamani, kwa waheshimiwa kutoa heshima zao za mwisho.Baada ya hapo msafara utaelekea nyumbani kwake Mbuzini kwa ajili ya Mazishi:''
kama kuna chcochote kitakacho badilika tutajulishana hapa hapa:
Ahsanteni Endelea kutembelea blog hii na Uwaambie wengine pia:
R.I.P Mzee Abraham Sepetu
TOA MAONI YAKO HAPA:

Sunday, October 27, 2013

TAARIFA JUU YA KIFO NA MAZIKO YA BABA WA WEMA SEPETU (MZEE ISSAC SEPETU)

Leo mapema tumepokea taarifa za kifo cha Baba mzazi wa Msanii nguli wa Filam nchini Tanzania Wema Sepetu Mzee Issac Sepetu (pichani), Ambae alikua anaumwa na amelazwa katika hospitali ya TMJ jiji Dar,Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Band Ya #COCONUT BAND ya Zanzibar Bwana RAY ambae ni  ndugu na wema sepetu ba mkubwa kwa ba mdogo, alisema mwili wa mzee sepetu kwa sasa umeshapelekwa katika Monchwari ya hospital Kuu ya Muhimbili:
Alipotakiwa kusema kuhusu wapi na nilini atazikwa mzee huyo: Bw; Ray alisema
Ray Mkurugenzi wa Coconut Band Zanzibar:
''kwa sasa tunawasubiri baadhi ya watoto wake waliyokuwepo marekani wafike, na wengine waliyokuwepo ujerumani na tunatarajia watafika kwenye jumanne, sasa wakifika tutazika kati ya juma nne au juma tano, na mzee tunatarajia atazikwa kwenye shamba yake Visiwani Zanzibar iliyoko shamba Mbuzini''
TOA MAONI YAKO HAPA:

Friday, October 18, 2013

WADAU WABARIKI NDOA YA WEMA SEPETU, DIAMOND:

Na Shakoor Jongo(GPL)
Wadau na mashabiki wa mastaa wawili nchini, Wema Sepetu wa Bongo Movie na Nasibu Abdul ‘Diamond’ wa muziki wa kizazi kipya, wamebariki ndoa ya wapenzi hao kwa kusema kuwa ni watu wanaoendana na kutegemeana kwa kiasi kikubwa.

Mwanzoni mwa wiki hii, Wema na Diamond walitupia katika kurasa zao za mitandao ya kijamii picha zao, ambazo zinaonekana zilipigwa eneo moja kwa simu moja na hivyo kuwapa wakati mzuri mashabiki wao ambao walionekana kupendezwa na uhusiano wao na kupendekeza waoane.
“Hii ndiyo couple bomba zaidi ya wasanii Bongo, kwa nini msioane? Mnapendeza sana jamani, ebu Diamond Platnumz achana na Penny bwana, huendani naye kwanza kuna mambo ya

Monday, October 14, 2013

JAY Z ALIVYOJICHANGANYA NA RAIA KWENYE TRENI:

 PICHA/Story TimesFm
Unaikumbuka ile surprise ya Mheshimiwa Mwakyembe kujichanganya kwenye treni ya abiria bila kutoa taarifa? Eeh..sasa Jay Z naye amefanya yake japo malengo yao yanatofautiana.
Rapper mwenye utajiri mkubwa na ulinzi wa kutosha amewasuprise fans wake wa London baada ya kujichanganya nao kwenye usafiri wa treni  wakati anaelekea kwenye tamasha lake katika eneo maarufu kwa burudani na sanaa ‘O2’ lililoko kusini mashariki mwa jiji hilo.
Ripoti toka katika nchi ya Malkia Elizabeth zinasema baba Blue Ivy ambae yuko jijini London ikiwa ni kati ya ratiba ya Magna Carta World tour, jumamosi jioni alipanda treni kama abiria wa kawaida akiwa ameongozana na

MAMA DIAMOND AINGILIA PENZI LA DIAMOND, WEMA


Stori: Mwandishi Wetu/Gpl
MAMA mzazi wa mkali wa ngoma ya Number One, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kasim ‘Sandra’ ameingilia kati penzi lililofufuka upya kati ya mwanaye na staa wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu.
Habari za chini ya kapeti zilitonya kuwa baada ya kuambiwa na kuoneshwa picha za Diamond akiwa kimahaba na Wema alikuja juu akidai kuwa hamtaki Wema kwa kuwa anamkubali zaidi Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda nyumbani kwake Sinza-Mori jijini Dar wikiendi iliyopita, bi’mkubwa huyo alisema kuwa kwa sasa hafahamu chochote kuhusu Diamond kurudiana na Wema zaidi ya kusikia kwa watu na kuona picha katika mitandao ya kijamii.
“Kuhusu Nasibu (Diamond) kurudiana na Wema, nasikia tu na kuoneshwa picha namsubiri Nasibu arudi kisha nikae naye ndipo nitatoa tamko,” alisema

Saturday, October 12, 2013

HAMMY B JAJI MPYA TUSKER PROJECT FAME TPF6:

 By EATV
Waandaaji wa shindano la kusaka vipaji vya kuimba lijulikanalo kama Tusker Project Fame hii leo limemtangaza jaji mpya wa mashindano hayo kutoka Tanzania.

Kwa mujibu wa Meneja wa Tusker Bi.  Bi Sialouise Shayo amesema kuwa jaji ambaye amechukua nafasi ya Mzee Zahir Zoro ni  Hermes J Bariki Hermy B.

Kwa upande wa mzee Zahir Zoro amesema kuwa amewapitisha vijana wanne ambao ana uhakika wataipeperusha vyema bendera ya Tanzania.


Naye Hermy B ameahidi kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwani ana uzoefu na mashindano hayo kwa muda mrefu.
TOA MAONI YAKO HAPA:

RAMA DEE: NAFASI YA R&B NI KUBWA SANA TANZANIA:

 by TIMESFM
Inawezekana we pia ukawa mmoja kati ya watu wanaoamini kuwa nyimbo zenye temple zinazokimbia sana ndio zinazopendwa zaidi Tanzania, au kama we ni msanii unawaza kuhama R&B ufanye  ngoma inayokimbia kama ya…, lakini Mwimbaji wa R&B Rama Dee yeye anaamini R&B ina nafasi zaidi nchini Tanzania na kwa anashauri usipokee maoni ya marafiki zako tu, ila uangalie pia watu duniani wanasikikiliza nini .
Hit Maker wa ‘Kama Huwezi’amefunguka kupitia kipindi cha The Chat cha Timesfm kinachoendeshwa na Ezden The Rocker kila jumamosi saa nne kamili asubuhi hadi saa sita kamili mchana.
“Nafasi ya R&B ni kubwa zaidi Tanzania, usiangalie tu rafiki zako wanasikiliza nini angalia watu duniani wanasikiliza nini halafu utapata jibu zuri zaidi, kwa hiyo R&B ina nafasi nyingi hata kama haina nafasi labda Tanga, ama labda haina nafasi Bukoba lakini ina nafasi zaidi Dar es Salaam na mikoa mingine na labda nchi nyingine tofautitofauti, kwa hiyo opportunities zipo nyingi sana, na wasanii wapo wengi sana wanafanya vizuri na wanafanya na live band, kama akina Damian, The Voice pia wapo, kwa hiyo mi naamini baada ya labda mwaka mmoja kila kitu kitaanza kutoka na kuonekana .” Amesema Rama Dee.
Wimbo wa Rama Dee aliomshirikisha Lady Jay Dee ‘Kama Huwezi’ umeshika nafasi ya 8 kwenye The Chat Countdown yenye nyimbo 20.

TOA MAONI YAKO HAPA:

Monday, October 7, 2013

Washiriki wanne wanaoiwakilisha Tanzania kwenye Tusker Project Fame

Tusker project fame mashindano ambayo yamewahi kuwapa ustaa wasanii kama Hemed PHD wa Tanzania yamefikia hatua ya washiriki kukaa kwenye academy ambapo matumaini ya Watanzania kufanya vizuri kwenye mashindano haya yapo mikononi mwa watu wanne.
Watu wenyewe ni  Angel, 23 yrs, Hisia 21 yrs, Tanah 21 yrs na Dubson 25yrs, unaweza kufatilia show ili ujue jinsi ya kuwapa support Watanzania hawa mtu wa nguvu ambao wako kwenye list ya zaidi ya wasanii 15 kutoka nchi mbalimbali za Afrika Mashariki.


TOA MAONI YAKO HAPA:

Sunday, October 6, 2013

ALBAM YA RAY C YAKAMILIKA RASMIN:

Nguli wa muziki wa Bongo Fleva Rehema Chalamila‘Ray C’amekamilisha albam ya nyimbo zake aliyokuwa akirekodi studio kwa miezi kadhaa.
 Kupitia mtandao wa instragram Ray C alisema kuwa….Album imekwishaaaaaaaaaaaaaaaaaa!Thank You Lord!
 Hivi karibuni msanii huyo alipost video na kuwaonjesha mashabiki wake ladha kidogo kati ya nyimbo zitakazopatikana kwenye albam hiyo ambayo haijajulikana itaitwa jina gani.
TOA MAONI YAKO HAPA:

Friday, October 4, 2013

20 PERCENT NA PRODUCER MAN WATER WAYAMALIZA KIHIVI:


Hakika Nyumbani ni Nyumbani tu ...Mwanamuziki 20 Percent ambayo miaka kama miwili iliyopita alikuwa ni tishio katika muziki wa Bongo Flava Hatimae ameamua kujirudi na kuondoa Beef walilo kuwa nalo na Producer wake ambaye ndio alikuwa anamtoa Man Water ...Wawili Hao wamekuwa kwa muda mrefu hawapatani kila mtu akisema mwenzake ndio mbaya ...ila leo wamekutana katika Ofisi za Magic FM na Kumaliza Tofauti zao na Kuhaidi kufanya kazi pamoja tena...20 Percent toka aachane na Producer huyo ameshindwa kabisa kufurukuta katika Game Hilo na kuonekana ameishiwa kabisa....Tunamuombea Arudi tena kama dhamani tupate Burudani Safi toka kwake;

TOA MAONI YAKO HAPA:

Tuesday, September 24, 2013

MBAYA WA AUNT AHENYA KORTINI

Yvonne Maximilian akiwa eneo la mahakama.
Stori: Musa Mateja GPL
Hatimaye yule mbaya wa mwigizaji wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel aitwaye Yvonne Maximilian (22) amenaswa na kuhenyeshwa kortini kisa kikiwa ni kumpiga chupa mwigizaji huyo.
Yvonne aliburuzwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar baada ya kukamatwa maeneo ya nyumbani kwake Kinondoni-Manyanya..........

Friday, September 13, 2013

DUUH!!!! STORY NZIMA YA KUFUMANIWA NA MKE WA MTU YA MZEE NGURUMO HII HAPA:

 From GLOBALPUBLISHER:
Stori: Brighton Masalu
SIKU chache baada ya kustaafu muziki, mwanamuziki mkongwe nchini, Maalim Mohamed Gurumo ‘Mzee Gurumo’ amekiri kupitia maisha mabaya ujanani ikiwemo kufumaniwa na mke wa mtu pamoja na uvutaji wa ‘sigara kubwa’ Ijumaa linaanika.

Akizungumza katika mahojiano na Kipindi cha Mkasi kinachorushwa na Runinga ya East Africa chini ya Mtangazaji, Salama Jabiri mwanzoni mwa wiki hii, Gurumo alisema miongoni mwa mambo mabaya ambayo hawezi kuyasahau maishani mwake ni pamoja na hayo.
KUFUMANIWA:
Katika sakata hilo, Gurumo alisema kuwa ilikuwa ni mwaka 1961 ambapo alikuwa na uhusiano na mke wa mtu ambaye aligoma kumtaja, ndipo siku moja wakiwa nyumbani kwa mwanamke huyo ‘wakiponda kirauli’ ghafla walisikia hodi na ndipo mwanamke huyo alipomwambia kuwa anayegonga mlango ni mumewe.
“Niliogopa sana, ikabidi nijibanze nyuma ya mlango, alipoingia tu...............

Wednesday, September 11, 2013

DUUUH!!! DIAMOND PLATNUMZ ASEMA KUANZIA LEO HATAKI COLLABO NA MTU YOYOTE KIBONGO BONGO;

Baada ya maneno mengi kutoka kuhusiana na ngoma mpya ya msanii DIAMOND PLATNUMZ, ameamua kuondoa ukimnya na kusema  kuhusiana na wote waliyosema kuibiwa ngoma hiyo kina mna moja ama nyengne,Diamond alifunguka leo alipokua akifanya interview na radio ya cloudFm jijini Dar- es - salaam,. Lakini pia  licha ya Diamond kukanusha madai hayo ambayo yalitolewa na Dayna na,Baba levo,Pia  alifika mbali na kusema kuanzia sasa hataki Collabo na mtu yoyote, ni bora afanye mwenyewe na wala hataki mtu aje amwambie anataka  Collabo labda kwa watu ambao anaheshimiana nao atafanya nao, lakini wengne wengine wasahau kabisa collabo na yeye,

Pia alielezea suala la kua na mtoto au kumtia mimba mwana denti wa FORM 4, kua suala hiyo c kweli na wala hana mtoto, laiti angekua nae asingemtelekeza angemfikisha kwa mama naseeb kisha baaas:
Hizo ni skando tuu za kutengenezewa na watu lkn hazina ukweli wowote ule: TOA MAONI YAKO HAPA:

HUU NDIO MJENGO WA MADEE MSANII WA BONGO FLEVA TANZANIA ULIYOMALIZA HIVI KARIBUNI:

Msanii wa bongo fleva T.Z HAMAD MADEE ameshare picha ya mjengo wake, ambao anaamini kuwa bila ya mziki pengine labda asingekua nayo so haina budi kushkuru mungu, madee amesema ngoma yake ya POMBE YANGU imesaidia sana kufanikisha kuimaliza ngoma iyo kwa sababu imempatia show nyingi sana na za ela ndefu,
Madee amesema nyumba iyo ipo maaneo ya Mbezi ya Kimara jijini Dar-es - salaam ambayo kwa sasa imemaliza kabisaa bado kuhamiwa tuu;

Kumbe BONGOFLEVA  inalipa kiasi hichi:
TOA MAONI YAKO HAPA:

(VIDEO) HII HAPA VIDEO YA DENTI AKIELEZEA MKASA MZIMA MPAKA KUPATA MIMBA YA DIAMOND:


TOA MAONI YAKO HAPA:

Sunday, September 1, 2013

HII HAPA NYIMBO YA DAYNA ANAYOSEMA AMEIBIWA NA DIAMOND PLATNUMZ (NUMBER ONE)

Juzi kati mkali wa music wa BongoFleva Diamond Platnumz alizindua rasmi ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la My Number One katika ukumbi wa Serena Hotel ambao watu wengi mashuhuri walialikwa kwenda kuiona video hiyo,
Kubwa lililoibuka kwa sasa ni kutoka kwa msanii wa kike wa Bongofleva pia, Dayna Nyange (Dayna), ameibuka na kusema kua wimbo ule ni wa kwake na msanii Diamond ameuiba, kwa mujibu wa Dayna anasema, Alimpelekea Diamond demo ya wimbo huo ili kuangalia uwezekano wa kumshirikisha lakin kadri siku zilivyokua zinakwenda Diamond alioneka kua bize sana, na mwisho wa siku, ngoma ndo iyo iliyozinduliwa juzi.
Licha ya hayo kikubwa na cha kushangaza ni kwamba Producer wa ngoma iliyozinduliwa ni SHEBY CLEVER na wa hii ya DAYNA ni huyo huyo, Je unafikiri kuna ufanano wowote kwenye ngoma izo;Hebu isikilize hii demo ya Dayna huku ukisubiri rasmi ngaoma hiyo ya diamond Kisha Utatuandikia maoni yako hapo chini kwa upande wako unahisi vip???:

TOA MAONI YAKO HAPA: