Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Monday, October 14, 2013

MAMA DIAMOND AINGILIA PENZI LA DIAMOND, WEMA


Stori: Mwandishi Wetu/Gpl
MAMA mzazi wa mkali wa ngoma ya Number One, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kasim ‘Sandra’ ameingilia kati penzi lililofufuka upya kati ya mwanaye na staa wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu.
Habari za chini ya kapeti zilitonya kuwa baada ya kuambiwa na kuoneshwa picha za Diamond akiwa kimahaba na Wema alikuja juu akidai kuwa hamtaki Wema kwa kuwa anamkubali zaidi Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda nyumbani kwake Sinza-Mori jijini Dar wikiendi iliyopita, bi’mkubwa huyo alisema kuwa kwa sasa hafahamu chochote kuhusu Diamond kurudiana na Wema zaidi ya kusikia kwa watu na kuona picha katika mitandao ya kijamii.
“Kuhusu Nasibu (Diamond) kurudiana na Wema, nasikia tu na kuoneshwa picha namsubiri Nasibu arudi kisha nikae naye ndipo nitatoa tamko,” alisema
mzazi huyo.
Mapaparazi wa Ijumaa Wikienda kadiri walivyozidi kumchimba mama mkwe huyo wa Wema ni jinsi gani anavyojisikia kuhusu tabia ya kubadilisha wanawake kama nguo, ikizingatiwa yeye ni mzazi haoni kama mwanaye anamfedhehesha alisema kuwa hayo ni maisha yake.
“Hayo ni maisha yake na mwenyewe kwa kuwa ameshazoea kuonekana katika magazeti kila wakati mi niongee nini wakati ndiyo maisha aliyojiwekea,” alimalizia kusema.
Imeandikwa na Shakoor Jongo na Musa Mateja.
TOA MAONI YAKO HAPA:

No comments:

Post a Comment