Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Monday, October 7, 2013

BARAFU ATOA YA MOYONI KUHUSU VIPAJI VYA MTAANI:

BY  filamucentral
MWIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood Suleiman Barafu ametoa kali pale alipoongelea soko la filamu la Bongo kwa kuwalaumu baadhi ya wasanii ambao hajawataja majina kwa kusema kuwa wasanii hao wapo katika tasnia ya filamu kwa muda mrefu kiasi cha kuona fani hiyo ni mali yao na hakuna anayestahili kuingia au kuigiza.
“Katika soko la filamu kuna tabia ya kubaniana, wasanii wakongwe hawataki kizazi kipya, kila sehemu wanataka wao pamoja na kuwa hawawezi, unamkuta mtu akipewa nafasi ya kukuongelea kwa bosi anakuponda mwanzo mwisho, sasa na sisi tunasema Maveterani wakae pembeni wasubiri mechi za mazoezi,”anasema barafu.
Msanii huyo ambaye pia ni muongozaji wa filamu amedai kuwa mitaani kuna vipaji vingi lakini vinanyimwa nafasia na wasanii wakongwe ambao hawataki kabisa kutoa nafasi kwa wasanii hao ili kuleta ushindani wa kweli katika tasnia ya filamu Swahiliwood, Barafu yupo mbioni kuachia filamu yake inayokwenda kwa jina la Dala dala kutoka kampuni ya Usambazaji ya Leo Media.


TOA MAONI YAKO HAPA:

No comments:

Post a Comment