Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Tuesday, September 24, 2013

MBAYA WA AUNT AHENYA KORTINI

Yvonne Maximilian akiwa eneo la mahakama.
Stori: Musa Mateja GPL
Hatimaye yule mbaya wa mwigizaji wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel aitwaye Yvonne Maximilian (22) amenaswa na kuhenyeshwa kortini kisa kikiwa ni kumpiga chupa mwigizaji huyo.
Yvonne aliburuzwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar baada ya kukamatwa maeneo ya nyumbani kwake Kinondoni-Manyanya..........

Yvonne akiwasili mahakamani.
Habari za ndani kutoka kortini zilieleza kuwa awali kesi hiyo ilikuwa isikilizwe na hakimu Agustino Mbando lakini baadaye kulitokea mabadiliko ambapo ilisomwa na Fundi Fimbo.
Aunt akiwasili mahakamani.
Akiwa mahakamani hapo huku Aunt naye akihudhuria kama mlalamikaji, Yvonne alishuhudiwa akipelekwa puta na polisi.
Hata hivyo, baada ya kesi hiyo kusomwa iliahirishwa hadi Oktoba 17, mwaka huu, itakaposikilizwa tena.
Akipanda mahakamani.
Agosti 26, mwaka huu, Yvonne anadaiwa kumjeruhi Aunt kwa chupa tupu ya bia na kumpasua mkono wa kushoto wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bilicanas, Posta jijini Dar.
...Akiwa mahakamani.
...Akitoka mahakamani.


No comments:

Post a Comment