Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Friday, September 13, 2013

REGINALD MENGI AJIBU MAPIGO, AKANA UFISADI:

 IMETOKA HABARI LEO:
MWENYEKITI Mtendaji wa Kampuni za IPP, Dk Reginald Mengi amejibu tuhuma zinazosambazwa kwa lengo la kumchafua katika jamii, zikimhusisha na ufisadi kwenye sekta za madini, gesi na mafuta. Pamoja na majibu ya shutuma hizo, Dk Mengi amesisitiza kuendelea na azma ya kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria waliohusika na uchafuzi huo, ili sheria ifuate mkondo wake.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Dk Mengi alisema hajapata kufanya udalali katika vitalu vya madini kama tuhuma hizo zinavyodai.
Alisema shutuma kwamba anafanya udalali katika vitalu vya madini na kuwa anajiandaa pia kufanya udalali katika vitalu vya mafuta na gesi, alizipokea kupitia barua pepe aliyotumiwa Septemba 7 na mtu aliyejitambulisha kama ‘CCM Tanzania’.
Alisema pamoja na..............
ujumbe huo uliokuwa na kichwa cha habari kisemacho: ‘ubinafsi/ufisadi wa Mengi na chuki/fitna kwenye maendeleo’ kutumwa kwake, pia ulitumwa kwenye vyombo vya habari, waandishi wa habari, mitandao ya kijamii na watu wengine wakiwamo wanasiasa.
Ujumbe huo pamoja na mambo mengine ulidai kuwa kampuni za Dk Mengi zinashikilia vitalu 59 vya madini vyenye ukubwa wa meta za mraba 3,752.37 ambavyo vimeshindwa kuendelezwa, huku Watanzania wakikosa mapato na ajira na kwamba sasa anataka vitalu vya gesi na mafuta ili afanye udalali pia.
Sehemu ya ujumbe huo ikizungumzia vitalu hivyo ilisema: “Amevishikilia, ameshindwa kuviendeleza. Watanzania wanakosa mapato na ajira … sasa anataka vitalu vya gesi na mafuta. Je huu ndio uzawa? Mengi hana uzawa bali ubinafsi. Anataka kufanya udalali wa vitalu vya rasilimali zetu. Waelezeni Watanzania ukweli huu." Akijibu, Dk Mengi alisema:
“Nimeona ni vema nitumie haki yangu ya kujibu, lakini kwa wale wanaohusika kusambaza taarifa hizo kuchafua jina langu, wajue kujibu kwangu hakuondoi haki yangu ya kuchukua hatua za kisheria.
“Kuingizwa kwa vitalu vya madini katika hoja ya gesi. Huo ni upotoshwaji wenye lengo la kututoa kwenye hoja ya msingi ya rasilimali yetu ya gesi. Sijawahi kufanya udalali kwenye vitalu vya madini.”
Alisema taarifa hizo ni za uongo na zimepotoshwa kutoka kikao cha Bodi ya Shirikisho la Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kilichofanyika Agosti 28 na kufuatiwa na mkutano wa waandishi wa habari kilichozungumzia rasilimali zilizopo nchini.
“Mambo mengi yalizungumzwa katika kikao hicho ikiwa ni pamoja na uwezeshaji wa Watanzania. Kuhusu uwezeshaji Watanzania, mambo muhimu matatu yalijadiliwa na kutolewa mapendekezo. Mambo hayo ni ununuzi wa umma, ardhi na uvuvi na gesi asilia.
“Kwenye mkutano na waandishi wa habari, mimi Mwenyekiti wa TPSF, niliwasilisha maoni kuhusu ununuzi wa umma, Makamu Mwenyekiti, Salum Shamte, aliwasilisha kuhusu sekta ya ardhi na uvuvi na Mkurugenzi Mtendaji, Godfrey Simbeye, aliwasilisha kuhusu gesi asilia.”
Mengi alisema TPSF ilisisitiza umuhimu wa ushirikishaji Watanzania katika uchumi wa gesi na kushauri kusitishwa ugawaji vitalu vya gesi hadi sera ya gesi itakapokuwa tayari.
Alisema wakati Simbeye akiwasilisha maoni yao, alisema TPSF itaomba kukutana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ili kuwasilisha mawazo na mapendekezo ya taasisi hiyo.
Alisema hata hivyo, siku chache baadaye Profesa Muhongo alijibu kupitia vyombo vya habari, kwamba mpango wa kugawa vitalu vya gesi na kuingia mikataba utaendelea huku akisema hana mpango wa kukutana na TPSF… ni kupoteza muda.
“Jambo la pili ambalo lilitokea ni mimi binafsi kushambuliwa kana kwamba maoni yaliyotolewa kuhusu gesi ni maoni yangu binafsi na si ya TPSF. Kuhusu tuhuma kwamba si mzalendo na ni mbinafsi, Mengi alijitetea:
“Ningependa kupuuza tuhuma hizo Watanzania wanafahamu ukweli. Vile vile ningependa kupuuza tuhuma za ubinafsi na kuwa sipendi maendeleo ya Watanzania wenzangu, kwa hili pia wanafahamu ukweli.
Alisema hapingi kuwapo wawekezaji wageni katika sekta ya gesi, lakini kuna mambo mawili anayapigania ambayo ni Watanzania kunufaika na rasilimali yao ya gesi na kuwapo kwa sera ya gesi inayotoa kipaumbele kwa Watanzania.
“Mimi napenda maendeleo ya nchi yangu; kwa hiyo hata siku moja siwezi kupinga uwekezaji au ubia na wawekezaji. Ninachosimamia ni manufaa kwa nchi yangu,” alisema Dk Mengi.

TOA MAONI YAKO HAPA:

No comments:

Post a Comment