Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Thursday, September 12, 2013

SANDRA ATOA WOSIA WA KIFO:

GLOBALPUBLISHER
 Stori: Gladness Mallya
MSANII wa filamu za Kibongo, Salma Salmini ‘Sandra’ ametoa wosia kuwa siku akiaga dunia azikwe siku hiyohiyo, maiti yake isilazwe.

Akizungumza na paparazi wetu, Sandra alisema alishawaambia ndugu zake pamoja na mumewe kuwa siku akiaga dunia azikwe haraka kwani imani yake inasema hivyo pia babu yake alimhusia hivyo.
Mwigizaji huyo alisisitiza kuwa, hata kama akiaga dunia asubuhi basi azikwe mchana kwa sababu familia yao ina asili ya Kiarabu mtu akifa anatakiwa kusitiriwa haraka iwezekanavyo kwani kuichelewesha maiti ni kuiongezea adhabu.
“Nimeshawaambia ndugu zangu na mume wangu kwamba ikitokea nimekufa maiti yangu isisubiri ndugu, jamaa na marafiki, hata kama mume wangu akiwa hayupo nizikwe tu,” alisema Sandra.

TOA MAONI YAKO HAPA:

No comments:

Post a Comment