Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Saturday, January 19, 2013

TAFF yaomba wasanii kujitolea


  Shirikisho la wasanii Tanzania 'TAFF' leo limefanya kikao ili kuweza kuangalia ni jinsi gani wanaweza kuendesha shirikisho hilo, kutokana na upungufu wa fedha walizokuwa nazo. Raisi wa shirikisho hilo Simon Mwakifamba, alisema shirikisho hilo halitegemei fedha kutoka Serikalini hivyo ni juhudi zao pekee ndizo zinazoweza kufanikisha kwao. Alisema pia sheria mbalimbali zimekuwa zikiwabana, hivyo huu ni wakati wa wao kuungana na kushikamana ili kuweza kupamba juu ya ufisadi wanaofanyiwa, kwenye tasnia yao kuanzia kwenye sheria ambao inawapa nafasi kubwa Wasambazaji kuwa na haki.
 
 Pia aliwataka wasanii kugangamala na kuungana pamoja ili kudai haki zao, katika kikao kilichofanyika Vijana, Kinondoni.
 Baadhi  ya wasanii wakiwa kwenye kikao
 Mkono na mwenzake, wakisikiliza kikao kutoka Al Riyam Production.
 Dr Cheni akiwa na Dino
 Steve nyerere akisikiliza mkutano
 Jack Wolper akiwa na wasanii wengine wakishikana mikono kuashirikia mshikamano



No comments:

Post a Comment