Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Wednesday, May 9, 2012

BASI LA MURO LATEKETEA KWA MOTO

Basi la kampuni ya  Muro Investment, T820BEY lillilokuwa likitokea Mwanza kwenda jijini Dar es Salaam, limewaka moto na kuteketea  kabisa maeneo ya Maseyu Mkoani Morogoro. Ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 1:15 usiku Mei 8,2012, haikusababisha madhara kwa abiria isipokuwa mali zao zote ziliteketea kwa moto
Mmoja wa wahusika wa basi hilo alidai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu ya umeme iliyolitokea gari hilo. Inadaiwa kuwa gari hilo lilipata hitilafu katika taa na walipofika mjini Morogoro walifanyia marekebisho na kuendelea na safari,  walipofika maeneo hayo ya Maseyu likashika moto.


 Hata hivyo gari hilo liliteketea kabisa kwani hakukua na zima moto wala msaada wowote wa kuliokoa

No comments:

Post a Comment