Baada ya kuwa kwenye rotation kali na video ya Fid Q, "sihitaji Marafiki", mwimbaji Yvonne Mwale anatoa video mpya. Wimbo unaitwa "Familia Yangu" ambayo ni single yake ya pili kutoka kwenye albamu yake inayoitwa "Kalamatila". Album hiyo imerekodiwa chini ya Caravan Records na tayari ipo sokooni. Inapatikani kwenye maduka ya vitabu "A Novel Idea", pamoja na iTunes.
Yvonne MwaleTitle: Familia YanguAlbum: Kalamatila (2012)Label: Caravan RecordsDirector: Matthias Krämer
"Familia Yangu" ni wimbo wa kwanza katika lugha ya kiswahili kutoka kwa Yvonne Mwale ambayo ametoka Zambia. Anasema: "Kwenye album yangu "Kalamatila" nimeimba nyimbo za lugha za nyumbani na kingerezi, ila nilipata wito wa kuimba katika lugha ya kiswahili baada ya kuhamia nchini Tanzania". Track hiyo inazungumzia changamoto inayo tokana na matatizo ya fedha kati ya mke na mume wake.......
Ingawa ni muda mfupi imepita tangu Yvone Mwale alizindua album yake ya "Kalamatila", mwimbaji huyu siyo chipukizi, bali ni msanii wa muda mrefu mwenye mafanikio mbali mbali katika game la mziki. Mwaka 2009 alishinda tuzo ya "Msani Bora wa Upcoming" Kwenye Zambia Music Awards. Baada ya kupata tuzo hilo alishinda tuzo ya Music Cross Roads (Afrika nzima) na bendi yaki Nyali Band na akaendelea kufanya tour nchi tisa Ulaya. Alivorudi alipata nafasi ya kupaform na Oliver Mtukudzi Malawi kwenye Tamasha inayoitwa "Lake of Stars".
Baada ya kufika Tanzania alipata nafasi kupaform na wasani mbali mbali wakiwemo, Mzungu Kichaa na Fid Q na wasanii wakimataifa kama, Maya Azucena, Bobby Rickets na Dobet Gnahoré. Mwezi uliyopita alishinda nafasi ya pili katika shindano la Mziki - Jahazi Jazz Music Competition.
Hivi sasa, Yvonne Mwale anarekodi na wasanii mbali mbali kutoka bara la Afrika na management yako wana andaa show kadhaa mwishoni mwa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment