Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Tuesday, June 26, 2012

Lindi wajiandaa na Epiq Bongo Star Search

SHINDANO kubwa la kutafuta, kuibua na kuendeleza vipaji nchini kwa sasa linaamia mkoani Lindi katika ukumbi wa Police Officers Mess Jumamosi ijayo.  Katika ukumbi huo washiriki wanatarajiwa kuanza usaili kuanzia saa moja asubuhi ambapo kabla ya kuanza kuonesha vipaji vyao mbele ya majaji.
Akizungumzia usaili wa Lindi Jaji Mkuu wa EBSS Ritha Paulsen alisema kuwa kama ilivyokuwa mkoa wa Dodoma na kisiwani Zanzibar  kwa mkoa wa Lindi wanatarajia kuona vipaji lukuki na aliwasihi wasichana kujitokeza kwa wingi.  “ Mimi ninaamini kuwa mkoa wa Lindi kuna vipaji yani kama ambavyo tumeona kwa maeneo mengine sasa kwa Lindi nadhani kutakuwa na ushindani mkali kwa kuwa wapo baadhi ya wasanii kutoka Lindi ambao wameweza kufanya vema katika medani ya muziki nchini”alisema Ritha.
Akizungumzia washindi waliopatikana Dodoma na Zanzibar Ritha alisema kuwa wamekuwa wakiimba vizuri na walionehsa uwezo mkubwa katika kupangilia sauti zao.  Naye Mkuu wa mawasiliano wa Zantel Awaichi Mawalla alisema kuwa Zantel ikiwa kama mdhamini mkuu wa EBSS 2012 kutokana na imani yao kwa wakazi wa Lindi katika kuendeleza sanaa anaamini kuwa mbali na kujitokeza kwa wingi ila pia watadhihirisha kuwa muziki ni asili yao.
Mpaka sasa majaji wa shindano hilo la EBSS 2012 wameshapata vipaji kutoka Dodoma na Zanzibar ambapo vijana 10 wamepatikana.

No comments:

Post a Comment