Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Thursday, June 7, 2012

Afande Sele aeleza sababu ya kutaka kwenda bungeni

Gwiji la Muziki wa kizazi kipya Seleman Msindi 'Afande Sele, baba Tunda' ameamua kuweka wazi sababu inayomfanya ajitose kwenye kinyanyiro cha kuwania Ubunge jimbo la Morogoro Mjini, kwakuwa watu ambao aliwaamini mwanzoni kwamba huenda wakawa chanzo cha kupata nafuu kwenye tasnia hiyo inayopendwa na vijana wengi lakini imekuwa tofauti sana Afande alisema miongoni mwa watu aliwaowategemea sana na ambao pia walikuwa kwenye tasnia hiyo ni wanamuziki Joseph Mbilinyi 'Sugu' na Captain John Komba, ambao aliamini huenda wangeleta mabadiliko kwakuwa wametokea kwenye fani hiyo. Alisema lakini tangu waingie huko, wamevaa uhusika wa kisiasa na kila jambo wamekuwa wakilipeleka kisiasa. Hali iliyompelekea kujipanga kwenda mwenywe bungeni, kupitia chama chochote cha upinzani, ambacho kitampa uhuru wa kuongea na kufanya yale ambayo anayahitaji yeye kwaajili ya watu wake. Pia alisema ananafasi nzuri ya kuwania akiwa mgombea binafsi, mwaka 2015 ambapo uchaguzi mkubwa utafanyika wa kuwania wabunge na raisi.

No comments:

Post a Comment