Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Wednesday, June 13, 2012

Diamond na Freemason

SIRI imefichukua kuwa madai kwamba ‘kichaa’ wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ ni memba wa jamii ya siri inayodaiwa kumwabudu shetani, Freemason a.k.a Wajenzi Huru zilianza kitambo lakini sasa zimeshika kasi baada ya kunaswa kwa picha inayomuonesha akisalimiana na mtasha kwa ishara ya Kifreemason.
Picha  ya tukio hilo lilijiri nchini Uingereza, mwaka jana Diamond alipokwenda  kwa ajili ya kufanya tamasha.
Inasadikiwa kwamba mavazi anayotumia mwanamuziki huyo kuwa ni meusi, yalifanana  sawia na yale ya mtasha, yanayoelezwa kuwa sehemu ya mavazi yanayotumiwa na jamii ya Freemason.
Ishara nyingine ya salamu ya wawili hao ambayo ilitengeneza nembo ya Freemason ya bikari kwa namna walivyogusanisha  vidole vyao.  
Wadau waliyoiona picha hiyo kupitiamtandao wa kijamii wa  Twitter, wanasema kwamba Diamond amekuwa na ishara nyingine nyingi za aina hiyo hali inayopelekea kuzua utata na kuamini kwamba ni memba wa jamii hiyo ya Siri.




No comments:

Post a Comment