Pages

MY NEW FILM TRAILER INAITWA ''DR MAX''

Saturday, October 12, 2013

RAMA DEE: NAFASI YA R&B NI KUBWA SANA TANZANIA:

 by TIMESFM
Inawezekana we pia ukawa mmoja kati ya watu wanaoamini kuwa nyimbo zenye temple zinazokimbia sana ndio zinazopendwa zaidi Tanzania, au kama we ni msanii unawaza kuhama R&B ufanye  ngoma inayokimbia kama ya…, lakini Mwimbaji wa R&B Rama Dee yeye anaamini R&B ina nafasi zaidi nchini Tanzania na kwa anashauri usipokee maoni ya marafiki zako tu, ila uangalie pia watu duniani wanasikikiliza nini .
Hit Maker wa ‘Kama Huwezi’amefunguka kupitia kipindi cha The Chat cha Timesfm kinachoendeshwa na Ezden The Rocker kila jumamosi saa nne kamili asubuhi hadi saa sita kamili mchana.
“Nafasi ya R&B ni kubwa zaidi Tanzania, usiangalie tu rafiki zako wanasikiliza nini angalia watu duniani wanasikiliza nini halafu utapata jibu zuri zaidi, kwa hiyo R&B ina nafasi nyingi hata kama haina nafasi labda Tanga, ama labda haina nafasi Bukoba lakini ina nafasi zaidi Dar es Salaam na mikoa mingine na labda nchi nyingine tofautitofauti, kwa hiyo opportunities zipo nyingi sana, na wasanii wapo wengi sana wanafanya vizuri na wanafanya na live band, kama akina Damian, The Voice pia wapo, kwa hiyo mi naamini baada ya labda mwaka mmoja kila kitu kitaanza kutoka na kuonekana .” Amesema Rama Dee.
Wimbo wa Rama Dee aliomshirikisha Lady Jay Dee ‘Kama Huwezi’ umeshika nafasi ya 8 kwenye The Chat Countdown yenye nyimbo 20.

TOA MAONI YAKO HAPA:

No comments:

Post a Comment