Waandaaji wa shindano la kusaka vipaji vya kuimba lijulikanalo kama Tusker Project Fame hii leo limemtangaza jaji mpya wa mashindano hayo kutoka Tanzania.
Kwa mujibu wa Meneja wa Tusker Bi. Bi Sialouise Shayo amesema kuwa jaji ambaye amechukua nafasi ya Mzee Zahir Zoro ni Hermes J Bariki Hermy B.
Kwa upande wa mzee Zahir Zoro amesema kuwa amewapitisha vijana wanne ambao ana uhakika wataipeperusha vyema bendera ya Tanzania.
Naye Hermy B ameahidi kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwani ana uzoefu na mashindano hayo kwa muda mrefu.
TOA MAONI YAKO HAPA:
No comments:
Post a Comment