(story/picha millardayo)
Ligi kuu ya soka nchini England imeendelea hii leo ambako michezo nane imepigwa .
Katika mchezo wa kwanza Manchester City waliwafunga Everton kwa mabao matatu kwa moja.
Everton walianza kufunga kupitia kwa Romelu Lukaku lakini Mabao toka kwa Alvaro Negredo , Sergio Kun Aguerro pamoja na bao la kujifunga la kipa Tim Howard yaliwapa Man City pointi Zote tatu .
Katika mchezo mwingine Liverpool wakiwa nyumbani kwao huko Anfield waliwafunga Crystal Palace 3-1 .
Mabao ya Liverpool yalifungwa na Daniel Sturdige , Luis Suarez na Steven Gerrard ambaye alifunga kwa mkwaju wa penati .
Bao pekee la Crystal Palace lilifungwa na Dwight Gayle .
Nao Newcastle United wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao wa mwisho dhidi ya Everton waliwafunga Cardiff City 2-1 .
Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Loic Remy ambaye amekuwa kwenye kiwango cha juu msimu huu alifunga mabao yote mawili ya Newcastle huku Peter Odemwingie akiifungia Cardiff bao pekee.
Fulham ambao wamekuwa kwenye mfululizo wa matokeo mabaya walizinduka usingizini na kuwafunga Stoke City 1-0 .
Bao pekee lilifungwa na mshambuliaji Darren Bent.
Mchezo kati ya Hull City na Aston Villa uliisha kwa sare ya bila kufungana .
Mchezo wa mwisho kwa Jumamosi uliwashuhudia Manchester United wakiwafunga Sunderland kwa mabao mawili kwa moja .Sunderland ndio walioanza kufunga kupitia kwa Craig Gadner kabla ya Adnan Januzaj hajaifungia United mabao mawili yaliyoipa pointi zote tatu.
TOA MAONI YAKO HAPA:
No comments:
Post a Comment